Monday, December 31, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MATOKEO YA SENSA NA WATU NA MAKAZI LEO IDADI YA WATU NA MAKAZI

0 comments
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo alizindua matokeo ya Sensa ya  Watu na Makazi  leo uzinduzi huo ulikwenda sambasamba na kutaja matokeo ya Idadi ya watu Tanzania  waliohesabiwa katika sensa ya watu na makazi iliyofanyika nchini nzima Rais alitaja idadi ya watu mara baada ya kuzindua jumla ya watu katika jamhuri ya Tanzania ni watu ni millioni 44 929 002  Ahasanteni 
Endelea Kusoma >>

KOCHA MPYA WA SIMBA AWASILI LEO

0 comments
 Kocha mpya wa klabu ya Simba Wekundu wa msimba hatmae amewasili jijini Dar es salaam leo kocha anafahamika kwa jina la Patrick Lieweig akitokea nchini Ufaransa amewasili muda wa saa 7,58 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalim Nyerere uliopo barabara ya pugu amelakiwa na katibu mkuu wa simba mtawala pamoja viongozi wengine pamoja na mashabiki wachache waliofika kwenye uwanja huo leo kocha huyo kwa mujibu wa katibu mkuu amesmea tarehe 1 januari 2013 atasaini mkata na klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi mara baada ya kuwasili kocha huyo aliongea na wandishi wa habari waliofika kwenye uwanja huo na kupata nasaha zake




Kocha mpya wa klabu ya Simba Patrick Liweig  kutoka nchini Ufaransa mara baada akifuatana mmoja wa kiongozi wa simba wakielekea kqwenye gari tayari kuelekea hotelini leo
Endelea Kusoma >>

Sunday, December 30, 2012

0 comments

MIKOCHENI CITY YATWAA KOMBE LA DIWANI


Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda akikabidhi kombe la Diwani kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa timu ya Mikocheni United Keneth Mutta (kulia) akichuana na Jerry Santo wa Mikocheni City katika mechi ya fainali ya kombe la Diwani iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni, Dar es Salaam juzi. City waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 4-3.

MAZOEZI YA KUAGA MWAKA 2012 NA KUKARIBISHA 2013

  Vijana wa jijini Dar es Salaam kutoka klabu za Jogging mbalimbali wakiwa kwenye mazoezi yaliyoanzia kwenye viwanja vya Tanganyika Pekaz Kawe jana, ambapo mazoezi hayo yaliambatana na bonanza kubwa la kuaga mwaka. Bonanza hilo liliandaliwa na Kawe Jogging.


Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan akiwapa mazoezi vijana wa vikundi mbalimbali vya Jogging wakati wa Bonanza la kuaga mwaka lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini Dar es salaam

 Mbunge wa Kinondoni Idd Azan akishiriki kwenye mazoezi hayo ambayo yalianzia Kawe kuzunguka hadi mbezi kupitia Lugalo na kurejea tena Kawe kwa kupitia Old Bagamoyo road.

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600 MWANZA

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania. (PICHA NA MDAU BALTAZAR MASHAKA)

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
Endelea Kusoma >>

Saturday, December 29, 2012

WASIFU WA JOHN MKETO

0 comments
 kwa niaba ya
Daniel Mshana
Marketing Manager
TANESCO LTD | Umeme Park-Ubungo
P.O.Box 9024 | Dar-Es-Salaam
Landline: +255 222 452 170 | Mobile: +255 784 257 046
website: www.tanesco.co.tz
[cid:image001.png@01CDE426.F45B80A0]


Ndugu habari? Please naomba pokea wasifu wa marehemu, mzee John Keto.

Alizaliwa Tarehe 15 August 1917 huko Muheza, Tanga

Alianza shule ya msingi mwaka 1922 akamaliza masomo ya secondary 1934.

Mwaka wa 1935 akaanza kazi ya ualimu huko St. Andrews Minaki hadi
mwaka 1938 alipo jiunga na chuo cha Makerere huko Uganda hadi mwaka wa
1940.

Baada ya masomo huko Makerere alirudi Minaki, kuendeleya na kazi yake
ya ualimu hadi 1949.

Badaye alienda Edinburgh Univesity kwa shahada ya Uzamili 1950-1954

Alirudi aliajiriwa shule ya secondari minaki 1954- 1958 kama makamu wa
mkuu  wa shule.

Baada ya hapo alichaguliwa kuwa mbunge wa TANU Tanga Province 1958-1960

Baada ya kumaliza nafasi hiyo ali teuliwa na Rais Mw. Nyerere kuwa
mwenyekiti wa Public Service Commission toka 1962 hadi 1964

Baada ya kutumika katika nafasi hiyo aliteuliwa  na \Mwalimu Nyerere
kuwa Post Master General(Director General) wa East African Posts and
Telecomunications makao makuu yakiwa Nairobi, Kenya 1964 hadi 1967.

Ilipoundwa East African Community, makao makuu ya posta yali hamishwa
huko Kampala na akaendeleya na kazi ile hadi 1976 alipo staafu.

Hapo ndiyo aliporudi Muheza kuboresha shule ya secondari Hegongo,
wilaya ya muheza tangu mwaka 1978 hadi 1985 aliporudi Korogwe
kupumzika.





________________________________
Endelea Kusoma >>

KATIBU MKUU WA CUF AKIWA MKOANI TANGA

0 comments
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi za chama kipya cha ADC zilizorejeshwa na baadhi ya wanachama  wa chama hicho na kujiunga na CUF katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga. katibu mkuu wa chama hicho yuko mkoani Tanga kwa ziara ya siku mbili katika kuhamasisha uhai wa chama hicho
Endelea Kusoma >>
0 comments


Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Tusipuuze

From

        Zitto Zuberi Kabwe 


   
Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Tusipuuze
by zittokabwe
Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Tusipuuze
Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.
Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?
Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.
Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.
Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.
Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?
Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?
Tuwasikilize watu wa Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.
Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.
Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera.  Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.
Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.

zittokabwe | December 29, 2012 at 10:57 AM

Endelea Kusoma >>

Friday, December 28, 2012

JOHN MNYIKA AZUNGUMZIA MAANDAMANO YA MTWARA KUHUSU GESI ISILETWE DAR

0 comments




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nitatoa kauli kamili baada ya kupata nakala ya risala iliyosomwa, hotuba zilizotolewa, ripoti za matukio tajwa na masuala ya ziada yaliyoibuliwa; katika hatua ya sasa natoa kauli ya awali kwamba:
MAANDAMANO NI MATOKEO YA UFISADI, UDHAIFU WA SERIKALI NA KUTOKUTEKELEZWA KWA WAKATI KWA MAAZIMIO YA BUNGE:
Mkutano na Maandamano ya wananchi wa Mtwara kutaka majibu toka  kuhusu manufaa ya miradi ya gesi  asili inayotoka katika maeneo yao ni matokeo ya madai ya ufisadi wa baadhi ya viongozi na udhaifu wa Serikali katika kuushirikisha umma katika michakato ya maamuzi ya  kisera na kitaasisi kuhusu rasilimali na miradi muhimu ya maendeleo.
Aidha, ni matokeo pia Bunge kutokuisimamia kikamilifu Serikali kwa niaba ya wananchi kwa mujibu wa ibara ya 63 ya katiba wakati serikali inapoacha kufafanua masuala yanayohojiwa na wabunge na inapokwepa kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu sekta ya nishati ikiwemo sekta ndogo ya gesi asili.
Iwapo Serikali ingezingatia maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwezi Julai 2011 na Julai 2012 miradi husika ya maendeleo ya gesi asili ingetekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi bila malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi katika mikoa yote inayohusika na miradi hiyo.
RAIS AHUTUBIE TAIFA KUHUSU GESI NA KUTUMIA MAMLAKA YAKE
Ili kurekebisha hali hiyo, nashauri Rais Jakaya Kikwete atumie hotuba yake kwa taifa ya mwishoni mwezi huu wa Disemba 2012 kueleza kwa umma undani wa miradi husika ya gesi asili  na manufaa yake kwa wananchi wa maeneo husika na nchi kwa ujumla; hatua ambayo alipaswa kuifanya tarehe 8 Novemba 2012 wakati wa uzinduzi wa mradi husika.
Aidha, Rais atumie mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ibara za 33, 34, 35, 36 kuagiza Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo, watendaji wengine wa Wizara hiyo na taasisi zake pamoja na watumishi wa umma mbalimbali wanaofanya kazi kwa niaba ya Rais katika maeneo ambayo miradi hiyo inatekelezwa kuchukua hatua ya kurekebisha udhaifu uliojitokeza na kutoa ufafanuzi kwa umma kwa kurejea pia masuala wabunge tuliyahoji kwa nyakati mbalimbali bungeni mwaka 2011 na 2012.

SERIKALI ITEKELEZE MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU NISHATI IKIWEMO KUREJESHA DOLA MILIONI 20.1 NA KUSHUGHULIKIA MADAI YA UFISADI
Kabla ya kufafanua kuhusu miradi iliyoanza hivi sasa, Rais au viongozi na watumishi wengine wa umma watakaozungumza kwa niaba yake waeleze mapato na manufaa ambayo wananchi wa maeneo husika na nchi kwa ujumla imepata kutoka gesi ilipoanza kuvunwa katika mikoa ya Kusini mwaka 2004 na hatua ambazo Serikali imechukua mpaka dhidi ya madai ya ufisadi wa baadhi ya viongozi katika mapato ya rasilimali hizo muhimu za taifa.
Serikali ieleze imefikia wapi katika kurejesha kiasi cha dola milioni 20.1 (zaidi ya Bilioni 30)  zilizopunjwa kifisadi katika mauzo ya gesi asili huku miradi ya maendeleo katika maeneo ambayo gesi hiyo imetoka kama Songosongo na maeneo mengine nchini ikiwa na upungufu wa fedha.
Ikumbukwe kwamba kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza bungeni tarehe 15 Julai 2011 kuhusu tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa mikataba katika sekta ndogo ya gesi inaoihusu pia Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAT) na kutaka kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza suala hilo.
Badala yake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliunda kamati ndogo ya iliyofanya uchunguzi uchunguzi wa masuala husika na taarifa kuwasilishwa bungeni mwaka 2011; hata hivyo mpaka sasa maamizio ya bunge kufuatia taarifa hiyo hayajatekelezwa kwa ukamilifu.


WAZIRI MUHONGO ATOE KWA UMMA MATOKEO YA UCHUNGUZI WA MIKATABA YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILI
Rais aagize Wizara ya Nishati na Madini iweke wazi ripoti na matokeo ya timu iliyoundwa na Waziri Muhongo kupitia upya kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ili udhaifu katika mikataba uliobainika mpaka sasa utumiwe na umma kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha sera, sheria, taasisi na mfumo mzima wa uingiaji wa mikataba kwa maslahi ya wananchi wa maeneo husika na taifa kwa ujumla.

NAENDELEA NA KUSUDIO LA KUTUMIA SHERIA KUPATA MIKATABA YA MKOPO WA DOLA BILIONI 1.225 NA YA MIRADI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA GESI MTWARA MPAKA DAR ES SALAAM
Kwa upande wangu hata baada ya maandamano na mkutano wa wananchi wa Mtwara walioufanya wa tarehe 27 Disemba 2012, nitaendelea kutekeleza kusudio langu nililolieleza tarehe 26 Disemba 2012 la kutumia kifungu cha 10 cha Sheria
ya ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kutaka nakala ya mkataba wa mkopo wa masharti kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.225 (shilingi trilioni 1.86) kutoka China.
Nitataka pia nakala za mikataba wa mradi wa miundombinu ya gesi asilia ambayo itahusisha ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na ujenzi wa bomba kuu la kusafirishia gesi asilia la inchi 36 kutoka Mtwara kupitia Lindi, Pwani hadi Dar es Salaam lenye umbali wa kilometa 532.
Hii ni kwa sababu mpaka sasa Wizara ya Nishati na Madini haijatekeleza pendekezo nililowasilisha bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwamba kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye Serikali ilipaswa kuwasilisha bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika.
Aidha, naitaka Serikali irejee  mapendekezo niliyotoa bungeni na kutoa maelezo kwa umma ya sababu za bomba hilo kujengwa kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam na kueleza kwa uwazi manufaa ya mradi huo na miradi mingine inayopaswa kutekelezwa katika mikoa ya Kusini kwa maendeleo ya wananchi husika.
Ikumbukwe kuwa tarehe 27 Julai 2012 nilieleza bungeni kuwa  pamoja na ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi asili Mnazi Bay na Songo Songo kama sehemu ya mradi huo; Serikali inapaswa kueleza ni miradi ipi inayoambatana na mradi huo ambayo imepangwa kuwanufaisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa MW 300 Mtwara na MW 230 wa Somanga Fungu (Kilwa).
SPIKA AELEKEZE KAMATI MBADALA YA KUISIMAMIA SERIKALI KWA NIABA YA BUNGE KUHUSU NISHATI NA MADINI
Kwa upande mwingine, utekelezaji wa mradi huo unaendelea bila kuwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ingepaswa kuishauri na  kuisimamia Serikali hivyo ni muhimu Spika wa Bunge akachukua hatua kutokana na barua niliyomwandikia mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2012 ambayo mpaka sasa haijajibiwa.
Izingatiwe kwamba katika barua hiyo nilitoa mwito kwa Spika atumie madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itayoshughulikia nishati na madini ikiwemo masuala ya gesi asili kwa sasa kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asili nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
28/12/2012
Endelea Kusoma >>

SHAHIDI ANGUKA MAHAKAMNI LEO ASUBUHI

0 comments


Shahidi wa kesi ya unyanganyi kutumia silaha Richard Edward Waziri mkaazi wa Tandale kwa Tumbo jijini Dar es salaam kushoto mwa picha akiteremsha kutoka katika chumba ch mahakama mkazi ya Kisutu leo baada ya kuanguka wakati aliposimamishwa ili kutoa ushahidi wake  ndipo alipoanza kuuguwa ghafla akitetemeka  mbele ya hakimu na watu waliokuwepo kumdaka na utoaji ushaidi kuahirishwa shahidi huyo alipata nafuu baada ya kuletewa chai na wahudumu wa kantini iliyopo mahakamani kisutu  alipokunywa akapata nafuu na kumpeka katika hospitali ya mnazimmoja leo picha akisindikizwa na jamaa yake
Endelea Kusoma >>

ESSI AONGOZA WALIOZIFUNGIA TIMU ZAO ZA TAIFA MAGOLI MENGI MWAKA 2012... ANAFUATIWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH

0 comments

ESSI AONGOZA WALIOZIFUNGIA TIMU ZAO ZA TAIFA MAGOLI MENGI MWAKA 2012... ANAFUATIWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH

Lionel Messi

MWAKA 2012, Messi hatimaye amekuwa nyota wa mabao wa Argentina baada ya kushindwa kwa miaka mingi kuhamishia kwenye timu yake ya taifa makali yake ambayo amekuwa akiyaonyesha Barcelona.

Maswali kuhusu tofauti ya kiwango cha Messi awapo Barcelona na anapoichezea timu ya taifa ya Argentina yanaonekana kupata majibu baada ya kuwasili kwa kocha Alejandro Sabella kwenye benchi la ufundi la Argentina.

Messi ndiye aliyeibuka kuwa mfungaji magoli mengi zaidi duniani ndani ya mwaka mmoja 2012 baada ya kufunga mabao 91, huku mabao 12 akiifungia timu ya taifa ya Argentina.

Huku akiwa amempita kwa goli moja Zlatan Ibrahimovic (ambaye ameifungia timu yake ya taifa ya Sweden magoli 11 mwaka 2012), Messi ametangazwa kuwa mchezaji aliyeifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi katika mwaka 2012, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwake kufanya hivyo. Kufikia sasa, takwimu za mabao za nyota huyo wa Barcelona kwenye timu yake ya taifa ya Argentina zimekuwa ni ndogo kulinganisha na zile za klabu.

Mwaka wake bora katika katika ngazi ya taifa ulikuwa 2007, ambapo alifunga magoli sita kwa  Argentina, yakiwamo mawili yake ya kwanza katika mechi moja, ambayo ilikuwa ni ya kirafiki dhidi ya  Algeria.

Magoli 12 ya Messi katika mwaka 2012 yanajumuisha 'hat-trick' zake mbili za kwanza kwa Argentina, alizofunga dhidi ya Brazil na Sweden.

Kama nyongeza, amefunga 'hat-trick' 19 akiwa na Barcelona, maholi manne katika mechi moja na magoli matano katika mechi nyingine moja.

Kutokana na David Villa kuwa mgonjwa baada ya kuumia vibaya Desemba 2011, Pedro ameibuka kuwa kinara wa mabao katika timu ya taifa ya Hispania. Nyota huyo wa Barcelona alikwenda kibahati kwenye fainali za Euro 2012 kutokana na kiwango chake wakati huo kuwa chini, lakini amefunga mabao saba katika mechi nane za timu ya taifa alizocheza mwaka huu.

RADAMEL FALCAO ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA 2012...NI TUZO INAYOTOLEWA KILA MWAKA NA GLOBE SOCCER... AWAPIKU LIONEL MESSI NA CRISTIANO RONALDO BAADA YA KUWAPIGA CHELSEA HAT-TRICK NA KUIPA ATLETICO MADRID TAJI LA SUPER CUP LA ULAYA... PIA ALIISAIDIA KLABU YAKE ATLETICO MADRID KUTWAA UBINGWA WA LIGI YA EUROPA MWAKA 2012

Radamel Falcao
Natishaaaaaa....! Radamel Falcao akishangilia baada ya kutupia bao.
DUBAI, Falme za Kiarabu
Straika wa klabu ya Atlético de Madrid ya Hispania, Radamel Falcao atakabidhiwa zawadi yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka 2012 ya Globe Soccer, ambayo hafla yake inafanyika jijini Dubai leo Desemba 28 na kesho (Desemba 29).

Falcao anayejulikana pia kwa jina la utani la 'The Tiger', alikuwa katika kiwango cha juu mwaka 2012. Alifunga jumla ya magoli 49 na pia kuisaidia Atlético kutwaa mataji mawili. Mcolombia huyu alithibitisha umuhimu wake katika kila michuano baada ya kufunga magoli mawili katika fainali ya Ligi ya Europa na kuipa ubingwa Atletico na pia akapiga 'hat-trick' katika fainali ya kuwania taji la Super Cup la Ulaya dhidi ya Chelsea na kuipa ubingwa klabu yake kutokana na ushindi wa 4-1.

Kwa sababu ya tuzo yake na pia kulazimika kuhudhuria hafla hiyo jijini Dubai, Falcao atachelewa kuanza mazoezi na wenzake klabuni Atlético.

Atlético imepanga kuanza kujifua kesho Jumamosi (Desemba 29) baada ya mapumziko ya Krismasi, lakini Mcolombia huyo anatarajiwa kuungana na kocha wake Simeone na  wachezaji wengine keshokutwa Jumapili (Desemba 30).

Mbali na Falcao, Atlético imeteuliwa pamoja na Chelsea, BATE Borisov na Juventus kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka. Miguel Ángel Gil Marín wa Atlético pia yuko jijini Dubai baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mkurugenzi Bora wa Klabu.

JOSE MOURINHO ATUA DUBAI NA KUSEMA HUU SIYO WAKATI WA KUJADILI HATMA YAKE REAL MADRID... KUKUTANA NA MARADONA, RADAMEL FALCAO, PLATINI

Mourinho (kushoto) akipokewa na wenyeji wake baada ya kutua katika uwanja wa ndege jijini Dubai jana.
DUBAI, Falme za Kiarabu
José Mourinho alitua jijini Dubai jana kushiriki katika mkutano wa saba wa michezo wa kimataifa (Dubai International Sports Conference).

Wakati akiwasili, kocha huyo wa Real Madrid aliulizwa kama ana mpango wa kuendlea kubaki na klabu yake ya sasa. Akajibu: "Sasa si wakati wa kuzungumzia hatma yangu", aliwaambia waandishi wa habari huku akitabasamu.

Mourinho ni miongoni mwa vinara wanaonogesha mkutano huo akiwa pamoja na Diego Armando Maradona, ambaye ndiye mwenyeji, rais wa UEFA, Michel Platini, ambaye ndiye mfunguaji wa mkutano na straika wa klabu ya Atlético de Madrid, Radamel Falcao
Endelea Kusoma >>

KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUU

0 comments


Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.

Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.

TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.

OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.

Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>

Thursday, December 27, 2012

ZITTO WAPAGAISHA MASHABIKI KATIKAMKESHA WA KRISMAS UKUMBI WA DAR LIVE

0 comments
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.akipagawaisha katika krismax dar live nakundi la  diamond
Endelea Kusoma >>
0 comments

KLABU YA URUSI ILIAMUANDALIA MESSI OFA YA KUFA MTU


KLABU ya Urusi ambayo haitajwi jina ilitoa ofa ya kutisha ya euro milioni 90 kwa Lionel Messi ili aihame Barcelona wiki chache zilizopita, imebainika.

Gazeti la Hispania la El Mundo Deportivo limesema kabla ya Messi hajamwaga wino katika mkataba mpya mapema mwezi huu, baba wa mchezaji huyo, Jorge, alifuatwa na klabu ya Urusi iliyokuwa tayari kumlipa euro milioni 30 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka mitatu.

Klabu hiyo ilikuwa pia imejiandaa kulipa ada iliyowekwa na Barca kama kipingele cha kuuvunja mkataba wake na klabu hiyo ya Catalunya ili nyota huyo akakipige Urusi.

Jorge Messi alimfikishia ofa hiyo mwanaye, lakini mchezaji huyo alikataa bila ya kusita na wala jambo hilo halikutajwa wakati wa maafikiano ya mkataba mpya na Barca.
Endelea Kusoma >>

WANANCHI WA MTWARA WAMEANDAMANA KUPINGA GESI ISIPELEKWE NJE YA MKOA HUO LEO

0 comments


  Wananchi wa mkoa wa Mtwara walifanya maandamano makubwa leo kupinga Gesi inayozalishwa mkoani mwao isipelekwe nje ya mkoa huo maandamano hayo yaliyokuwa ya amani wakipita katika mitaa mbalimbali wananchi hao ambao wanalani kwa gesi yao kupelekwa Dar es salaam na mikoa mingine wanadai kwanza waanze kupewa wao katika mkoa wao halafu ndipo ipelekwe nje ya mkoa maandaamano yalijumuisha vyama vya siasa vyote kasoro chama Tawala tu hakikushiriki maandamano hayo walitaka yapokelewe na mkuu wa mkoa lakini mkuu huyo alichomoa 

Endelea Kusoma >>
0 comments

TIGO YATANGAZA OFA KUPIGA SIMU NNJE YA NCHI.


Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Bulla Bona, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ofa ya msimu wa sikukuu ya hudumuma ya Xtrime Pack itakayowawezesha wateja kupiga simu kwa gharama nafuu zaidi kwenye nchi 6, UK, USA, Canada, India, Hong Kong or China, dakika 5 kwaTsh 150.Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua picha wakati wa kutangaza ofa hiyo jijini Dar es Salaam leo.Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Bulla Bona, akizungumza
Endelea Kusoma >>

Wednesday, December 26, 2012

YANGA YAPIGWA MWELEKA NA TUSKAER 1 -0

0 comments
mshambulioaji watimu ya yanga george Banda akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Tusker kutoka nchini kenya wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kqwenye uwanja wa taifa  katika mchezo huo timu yaYanga imefungwa bao moja kwa bila
Beki watimu ya Tusker Chikokoti akikjaribukumzukia
bahanuzi akipambana bekiwa tusker
Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu