Wednesday, May 22, 2013

HALI HALISI YA MTWARA LEO

WAANDISHI WETU MTWARA
HALI ya usalama katika Mji wa  Manspaa ya Mtwara Mikindani imezidi kuwa tete kufuatia wananchi kusitisha huduma za kijamii kwa ajili ya kusikiliza bajeti ya wizara ya nishati na madini.
Hali hiyo imejitokeza majira ya asubuhi ambapo maeneo ya mjini hapakuwa na watu huku magari ya polisi na zima moto yakiwa katika doria zao za kawaida.
 Jeshi la polisi lilimwaga unga wa kuwasha ulizagaa katika makazi ya watu huku wakazi wa maeneo hao wakipata madhara kutokana na kuwashwa.
Kufuatia hali hiyo wananchi walilalamikia kitendo hicho cha askari hali iliyopekea wananchi kushikwa na hasira.
Wananchi wakiwa tayari wamejiandaa kusikiliza bajeti ya wizara ya nishati na madini katika hali isikuwa ya kawaida kituo kinachjorusha matangazo ya bunge cha shirika la utangazaji cha TBC, majira ya saa mbili kilikatisha matangazo yake kwa mji ya Mtwara hali iliyoibua sintofahamu kwa baadhi ya wananchi.

“Ona sasa hata matangazo ya bunge wameketa, wanamaanisha nini wakati sisi tunahitaji kufahamu hatma yetu” Alisema Ali hamis mfanyabiashara wa soko kuu mjini hapa.
Hata hivyo matanagazo ya bunge yalirejea majira ya saa 3:55 ambapo wananchi walikuwa  wakisikiliza bunge la bajeti majumbani mwao.

Majira ya saa 6 askari wakiwa katika doria maeneo ya soko  kuu vijana walizunguka huku na huku wakiwazomea maaskari na kurushiwa mawe.

Barabara Kuu ya Mtwara Dar katika maeneo ya Mkanaledi mjini hapa vijana wenye umri wa miaka 12-14  walifunga barabara ambapo polisi walilazimika kwanda na kufungua barabara hiyo.

Katika maeneo ya magomeni mjini hapa, wananchi wa lichoma mataili barabarani hali iliyosababisha halia ya taharuki na kuwalazimu jeshi la polisi kuingilia kati kuzima moto huo.

shule zimefungwa kwa siku hazijulikani  wamelazimika kufunga shule kwa siku mbili mpaka hapo hali itakapotulia.

Huku katika shule ya msingi Chokongola Mjini hapa,  mwalimu,Joseph  Kandeo, aliiambia Nipashe kuwa  wamelazimika kuwarudisha watoto nyumbani kwa muda wa siku mbili  mpaka hapo watakapotangaziwa.

Ofisi ya Chama cha mapinduzi wilaya ya Mtwara imechomwa moto, huku Ofisi ya Mbunge wa  Mtwara Mjini Husnein Murji iliyoko Mikindani ikichomwa moto, pamoja na nyumba ya  mwandishi wa habari wa kituo cha utangazaji cha TBC Mkoani hapa, Kasimu Mikongolo imeteketezwa moto na wananchi.

Aidha pia wananchi hao wamechoma Mahakama ya mwanzo ya Mitengo pamoja na Ofisi ya kata hiyo ya Mitengo.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida waandishi wa habari Mkoani hapa wamepata wakati mgumu kufuatia baadhi ya wananchi kudai kuwa hawaandiki taarifa kwa usahihi na  kudai kuwa waandishi wa habari wapo kwa ajili ya kutetea serikali.

“Hawa wapo pamoja na serikali,wala hawapo kwa ajili ya kutetea wananchi, hawa wanastahili kupigwa” zilisikika sauti za baadhi ya kundi la watu wakisema

Kufuatia hali hiyo waandishi wa habari  walijificha kunusuru maisha yao huku waandishi wakilazimishwa kutoa vitambulisho vyao.
Baadhi ya wandishi wa habari walinusurika kichapo baada ya kukosa vitambulisho

Hali ya Mji wa Mtwara ni tete hakuna aina yoyote ya usafiri, hakuna gari linaloingia wala kutoka, boda boda, bajaj, tax, magari ya watu binafsi yamepaki.

Salum Juma, mwendesha boda boda Mkoani hapa alisema kuwa alipokea vitisho kutoka kwa wananchi wakimtaka kuacha kupakia abiria ikiwa atalazimisha pikipiki yake itachomwa moto.

Mabasi yanayotoka mikoani yameshindwa kuingia kutokana na hali tete mjini hapa, hivyo abiri wote wapo Mkoani Lindi Wakihofia usalama wao.
Diwani wa kata ya Likombe  Mukhusin Komba  kuwa  wananchi walivamia nyumba yake na kuvunja duka, kuiba vitanda vitatu,na  magodolo manne.

Majira ya saa 5;30 asubuhi, Jeshi la polisi limelazimika kutawanya vikundi vya  wananchi kwa mabomu.

 Hata hivyo Wananchi walionekana wakijibizana na jeshi la polisi kwa kuponda mawe, hali iliyowalazimu jeshi la polisi kutumia risasi za moto pale wanapozidiwa.

Hakuna huduma yoyote inayotolewa kwa siku hii ya leo, ambapowafanyakazi wa serikali pamoja na mashirika binafsi wameonekena wakiwa ofisini peke yao,hali iliyowatia wasiwasi kwa baadhi ya makampuni binafsi na mashirika kulazimika  kufunga ofisi zao.
Kwa upande wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Ligula,  Mohamed Kodi alithibitisha kupokea maiti ya mtu mmoja ambaye amefariki katika vurugu hizo.
Alibainisha kuwa katika hospitali hiyo wamepokea majeruhi kadhaa Ambao idadi yao hajafahamika wamelazwa katika hospitalini hapo.





Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu