2


SI LA KULIKOSA

Wednesday, July 17, 2013

Ajali nyingine tena, Air Bus lapinduka Maseyu

Photo: Basi la Airbus likielekea Dar-es-salaam kutokea Tabora
Basi la Airbus likiwa safarini. Moja ya mabasi hayo limepata ajali jioni hii

ABIRIA 23 waliokuwa wakisafiri na basi la Air Bus linalofanya safari zake kati ya Tabora na Dar wamejeruhiwa wanne kati yao vibaya baada ya basi hilo kupinduka eneo la Maseyu, mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na Radio One hivi punde ni kwamba basi hilo lilipinduka kutokana na mwendo kasi wakati likijaribu kuyapita malori na kupoteza muelekeo kabla ya kupinduka.
Taarifa hizo zinasema kuwa, majeruhi wameumia vibaya maeneo ya kichwani, kifuani na miguuni na wamekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, huku wanne akiwemo dereva wa basi hilo wenyewe wakiwahishwa jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kati ya abiria haop waliojeruhiwa 13 wamelazwa hospitali hiyo ya mkoa wa Morogoro, na kwamba taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa ili kujua kinachoendelea, ingawa mpaka sasa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu