Wednesday, July 10, 2013

AJALI YA BASI NA CENTER USO KWA USO

WATU 11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Taqwa walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
Ajali hiyo mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika mtelemko wa mlima Mambi katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani Mbarali ikihusisha basi la Kampni ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na lori aina ya Center lenye namba za usajili T 175 BRA.
Baadhi ya watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa wakati basi hilo likiwa kwenye mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya Center ambalo lilikuwa likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa limesimama kando ya barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso na kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu