Saturday, July 20, 2013

AJALI YAUA WATU WANNE DODOMA JAN

WATU wanne wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Najimunisha lililokuwa likitokea Dar es Saalam kwenda Mwanza kupasuka tairi la mbele na kwa dereva kupinduka katika eneo la Mbande Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Kaimu Kamannda wa Polisi Mkoa w Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda alisema tukio hilo lilitokea jana saa saba na nusu mchana.
Alisema basi hilo lenye namba za usajili T.491 AUF aina ya Scania Busi lilipofika katika mteremko maeneo ya Mbande likiwa katika mwendo kasi lilipasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kupelekea dereva kushindwa kulimudu.
Alisema kutokana na hali hiyo basi likaacha njia na kuingia msituni, hatimaye kugonga kisiki cha mbuyu na kupinduka.
Kaimu Kamanda alisema kufuatia ajali hiyo watu wanne  walipoteza maisha akiwemo dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina la Hussuin Mashiba mwenye umri kati ya miaka 40 na 42.
Aliwataka Watu wengine watatu waliopoteza maisha Rashid Boyo (42) ambaye alikuwa kondakta wa gari hilo, na mkazi wa Mwanza , Fanuel Mganji mwenye miaka kati ya 28 na 30, Fundi na utingo wa basi hilo. Emmau Tegani ambaye ni Muuza maji na mkazi wa Mbande ambaye alipanda basi hilo kwa lengo la kuuza maji.
Aidha kufuatia ajali hiyo, watu kumi wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu, watatu kati yao wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa. Majeruhi hao wote watatu ni wa kiume wametajwa kuwa ni Rabiel Masue (27), Mkazi wa Mwenge  Dar es Salaam, Charles Joseph (28) Mkazi Kapri Point, Mwanza na Burton Kimaro (27) Mkazi wa Mwanza.
Alisema majeruhi wengine saba ambapo  watatu kati yao wakiwa ni wanawake wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma.
Kufuatia tukio hili la ajali, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo na wote watakapopatikana na makosa watafikishwa mbele ya sheria.
Kaimu Kamanda alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa rai kwa madereva hususan wa magari ya abiria kuzingatia miiko na maadili ya udereva na kutoenda mwendokasi. Aidha linawataka abiria, iwapo dereva atakuwa anakwenda mwendokasi, watoe taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri wanapowaajiri madereva, wahakikishe kuwa wamewasaili kikamilifu na wanakidhi vigezo vinavyohitajika kisheria.
Kwa upande wake, Mganga  Mkuu Mfawidhi wa  hospitali ya mkoa wa Dodoma Dk,Nassoro Mzee alisema majeruhi walianz kupokelewa kuanzia saa nane mchana jana.
Kwa upande wao majeruhi waliyolazwa kwenye hospital hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali ni kupasukaa kwa tairi la mbele na wakati huo dereva alikuwa  mwendokasi.
Mmoja wa majeruhi John Kazungu (25) alisema kuwa licha ya pancha lakini pia dereva  alikuwa katika mwendo wa kasi hali iliyosababisha ajali hiyo.
“  Mimi Nilikuwa upande wa Kondakta  mara nikasiki kishindo kikubwa na kuanza kuona gari yetu ikaacha kwa kupoteza muelekeo  wa njia  na kupinduka  toka hapa sikujua kinacho endelea ndio nimejikuta hapa,  ” alisema  Kazungu.



Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu