Saturday, July 20, 2013

BAADA YA KUMKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO RAIS OBAMA

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Leberata Mulamula akiwa na Rais wa Marekan Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho Alhamisi Julai 18, 2013 katika Ikulu ya marekani "White house" na kisha kufuatia na tafrija ya kumpongeza iliyofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. (Picha kwa hisani ya Swahili Tv)

KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA AHAMASISHA MKAKATI WA POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI WILAYANI MPWAPWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akiachana  na gari lake na kuungana na  na kikundi cha ulinzi shirikishi kilichofahamika kwa jina la Mwananzele kilichopo katika kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, waliokwenda kumpokea akiwa njiani kabla ya kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuongea na wanakijiji hao masuala mbalimbali yahusuyo ulinzi na usalama wa watu na mali zao.

Wazee wa Kimila wa Kijiji cha  Mbori katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa, wakimvika vazi rasmi na kumkabidhi mkuki Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime Kama ishara ya kumtambua rasmi kuwa kamanda na mlezi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha mwananzele katika kata hiyo.
Wanakijiji wa Mbori  katika Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza kwa makini  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, ambaye alikuwa akiwahutubia wanakijiji hao kuhusu miradi mbalimbali Iliyopo katika mpango wa Polisi jamii na Ulinzi shirikishi juu ya umuhimu na faida zake kwa jamii hiyo.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akishiriki na kikundi cha ulinzi shirikishi kilichofahamika kwa jina la Mwananzele kilichopo katika kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, waliokwenda kumpokea akiwa njiani kabla ya kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuongea na wanakijiji hao masuala mbalimbali yahusuyo ulinzi na usalama wa watu na mali zao.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, akifanya Ukaguzi kwa askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha Mwananzele cha kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuangalia na kujua ukakamavu wao uko imara kiasi gani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, akifanya Ukaguzi kwa askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha Mwananzele cha kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuangalia na kujua ukakamavu wao uko imara kiasi gani.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu