Wednesday, July 24, 2013

Chelsea bado yamng'ang'ania Rooney

Wayne Rooney
KLABU ya Chelsea inajiandaa kuongeza dau la kumnasa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney licha ya United kusisitiza kuwa nyota wao huyo HAUZWI.
Kwa mujibu wa duru za kimichezo toka nchini England zinasema kuwa Chelsea wanajiandaa kuweka mezani Pauni Milioni 40 ili kumnasa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo amekuwa hana furaha ndani ya United na imedaiwa kuwa anataka auzwe, lakini uongozi unaweka ngumu.
Chelsea chini ya kocha wake Jose Mourinho imekuwa ikimmezea mate mshambuliaji huyo tegemeo wa England na imeendelea  kusisitiza kuwa inahitaji saini yake kwa sasa.
Arsenal pia ilitajwa kuwa katika mbio za kumnasa mkali huyo wa mabao, ikijitapa wana uwezo wa kumlipa mshahara wake wa pauni 250,000 kwa wiki.
Kuna uwezekano mdogo kwa United kulegeza msimamo wake licha kwamba huenda dau hilo litawavutia baada ya timu yao kuandamwa na majeruhi kabla ya kuanza kwa Ligi.
Mfungaji Bora wa EPL, Robin van Persie aliumia wakati United ikilala Asia kwa mabao 3-2 huku Danny Welbeck akitajwa kuwa majeruhi hali inayomtisha kocha David Moyes
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu