Sunday, July 28, 2013

COAST UNION YAITUNGUA SIMBA BAO 1-0 BILA MAJIBU LEO MKWAKWANI TANGA

KIKOSI CHA COAST UNION
TIMU ya soka ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kuvitisha vigogo vya soka nchini ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu  wa 2013-2014 baada ya jioni hii kuizima mdomo Simba na kushinwdwa kunguruma  baada ya kunyukwa  bao 1-0 katika mechi ya kirafiki.
Pambano la leo lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga ilishuhudiwa hadi wakati wa mapumziko kukiwa hakuna mbabe yeyote baada ya timu zote kutoshana nguvu ya kutofungana.,
Hata hivyo katika kipindi cha pili Coastal walionyesha ilivyopania msimu ujao kwa kuwakimbiza Simba na kujipatia bao pekee lililowekwa kimiani na mchezaji wao mpya toka Kenya,  Crispian Odula Odwenye aliyefunga katika dakika 54.
Hicho ni kipigo kingine kwa Simba katika mechi zake za karibu za kirafiki za kujipima nguvu na inamfanya kocha wake, King Abdallah Kibadeni kurekebisha mapema kikosi chake kabla ya ligi.
 

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu