Monday, July 22, 2013

IGP AKIWA UNGUJA NA PEMBA


Wanafunzi wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa  upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani, Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Hapsa Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar baada ya IGP Saidi Mwema kufanya  uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

LIGI KUU YA VODACOM 2013/2014 KUANZA AGOSTI 24

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- attached).
TAIFA STARS KWENDA KAMPALA J5
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.
Boniface Wambura
Ofisa Habari

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu