Saturday, July 27, 2013


IRINE CHEPTAI WA KENYA AANGUKA NA KUZIMIA BAADA YA KUMALIZA MBIO ZA MITA 3,000

Daktari wa kwanza kabisa kumkimbilia Irine Cheptai akihaha kuuzindua moyo wake baada ya kuzimia, alipokuwa akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London jana.
Collapsed: Irine Chebet Cheptai was rushed to hospital after collapsing following the 3,000m
Jopo la Madaktari wakihangaika kumpatia huduma ya kwanza Irine Cheptai, alianguka na kuzimia wakati akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki.
treatment: Chebet Cheptai left the track unconscious but, according to reports, later regained consciousness in hospital
Cheptai akiwa ametungikiwa mtungi wa hewa ya oksijeni, baada ya kuanguka na kuzimia kutokana na shambulio la moyo. Hata hivyo alikuja kurejewa na fahamu zake akiwa hospitali.
The Kenyan finished 11th in the race
Cheptai (wa pili kulia) akikimbia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London.

LONDON, England
Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia

MKIMBIAJI wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya, Irine Chebet Cheptai jana alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na mshituko wa moyo kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita 3,000.

Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia.

Madaktari waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha kumtundikia mtungi wa Oksijeni, ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo zilipasha kuwa alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.

Tukio lake limeshtua wengi kutokana na kukimbia katika mbio fupi kulinganisha na zile alizozoea za mita 5,000, ambazo ameshiriki Diamond League mara mbili msimu huu, na anakumbukwa kwa rekodi yake ya dakika 14:50.99 jijini Shanghai, Mei mwaka huu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu