Thursday, July 4, 2013

Kesi dhidi ya maafisa wa Chadema yatupiliwa mbali

Kesi dhidi ya maafisa wa Chadema yatupiliwa mbali

Mwita Waitara

KWA mara nyingine Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida, ilitupilia mbali kesi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyokuwa ikiwakabili, Mwita Waitara, Afisa sera na utafiti Makao Makuu na Mshauri wa Chama hicho Dk Kitila Mkumbo,

Kesi hiyo ilitupiliwa mbali baada ya Mashahidi wa Serikali kushindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washitakiwa, waliyomtukana Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Mchemba, yaliyodaiwa kutolewa na Washitakiwa.

Sababu nyingine ya kutupilia mbali kesi hiyo ilielezwa kuwa ni upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Nchemba, aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yalimuathiri.

“Washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali wameshindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa”.alisema Masham Hakimu wa Mahakama hiyo.

“Upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri”.alisema Hakimu.

Alisema, Kushindwa kwa Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na hivyo Mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa, alisema hakimu huyo.

Awali Washtakiwa hao, walidaiwa kutenda kosa hilo Julai 14, mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba, ambapo Chadema kilikuwa na mkutano wa hadhara.

Wakati ikisomwa hukumu hiyo, alikuwepo Wakili wa Washitakiwa, Tundu Lisu, ambapo Hakimu Masham alisema washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washitakiwa.

Kesi hiyo ambayo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, iliibua minong’ono jambo ambalo imedaiwa lilikuwa likimkera Hakimu wa kesi hiyo.

Wadau wa mambo ya kisheria wamekuwa wakihoji maswali mengi yasiyokuwa na majibu kwamba, inakuwaje baadhi ya viongozi wa Chama tawala wanawashaiwishi watu kufungua kesi zenye maslahi yao binfasi halafu siku ya kesi hawafiki? Je ni njia ya kuwasumbua watu au ni kuwapuuza Mahakimu?

Wengi wao wamekuwa wakiwatafsiri kuwa wanafanya hivyo wakijua wao ni chama tawala hivyo wanafanya ili kuwakomoa na kuwapa usumbufu wanaotuhumiwa kwa maana ya kuwafanya wazibe midomo ya kuwatetea wananchi?

Mwananchi ambaye alikuwepo mahakamani hapo na yeye akiwa na kesi alisema, anawashauri mahakimu wakate kudharauliwa na Viongozi wa Sampuli hizo, amabo wanawashikiza watu wafungue kesi kwa kulinda heshima zao, halafu wahusika hawafiki mahakani.

Amedai, kwanza kitendo hicho kinawadharirisha wananchi ambao wanabebwa kama debe tupu likisubiri hewa liwekwe kitu, ambapo wahusika wanaoona kesi zinawaendea kombo wanajificha na hivyo kuwaacha wao kama chama wakiadhrika.

Mama ambaye alikuwa mahakani hapo akiwa na kesi ya Miradhi alisema, tabia inayofanywa na viongozi hao, inachezea muda na fedha ambayo ni kodi ya wananchi, lakini akadai badala ya Mahakimu hao kufanya kazi ya kusikiliza kesi za wananchi zenye msingi wa kuwasaidia, wanapoteza muda kwa mambo yasiyo na maana.

Aidha Mwanaharakati aliyeomba asitajwe alisema, baadhi ya Viongozi na Watanzania wasipofuta mawazo ya kufanywa watumwa Punda au Ng’ombe, baadhi ya wanasisa watawachezea hivyo wasikubali kuwafanya vihongwe, huo wao wakijificha kwenye mapambano mfano kesi hizo.

Kuelekea Usiku wa Matumaini; Wabunge, Wasanii, Mabondia watambiana




Mratibu wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, Abdallah Mrisho 'Abby Cool' (katikati), akiongea na wanahabari leo kuhusu burudani zitakazokuwepo siku hiyo.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala (katikati), akielezea jinsi timu yake ya Simba (wabunge) watakavyoigaragaza Yanga katika mechi yao.
Mbunge wa Igalula, Dkt. Athumani R. Mfutakamba (wa kwanza kushoto), akiwawakilisha wabunge wa Yanga katika mkutano huo.
Mwanamuziki 'Diamond Platnumz' akieleza jinsi atakavyomfunika msanii Prezzo kutoka Kenya.
Afisa Masoko kutoka kampuni ya simu za mkononi Tigo ambao ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo, Alex Msigala akiongea na wanahabari jinsi kampuni yake ilivyojipanga kufanikisha Usiku wa Matumaini 2013.
Meneja Uhamasishaji Rasilimali kutoka TEA, Doreen Shekibula (katikati), akipongeza waandaaji wa Tamasha hilo.
Jacob Steven (JB) akionyesha jinsi atakavyomwinua Mhe. Idd Azzan katika mpambano wao wa ndondi.
Msanii Ray Kigosi (katikati) akijinadi kuwa atamvunja taya Mhe. Zitto Kabwe siku hiyo.
Mwakilishi wa Bongo Fleva, H-Baba akielezea jinsi timu yake itakavyotoa kichapo kwa wapinzani wao wa Bongo Muvi.
Jacqueline Wolper (katikati) akimtumia salamu Mhe. Halima Mdee kuhusu kichapo atakachomshushia siku hiyo.
...Akionyesha jinsi alivyojipanga kumchapa Mdee.
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akielezea alivyo fiti kumkabili JB.
Bondia Thomas Mashali akitoa tambo zake kuwa atampa kichapo Patrick Amote kutoka Kenya.
Bondia Francis Miyeyusho akiwaeleza wanahabari alivyo tayari kumkabili bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi bendi yake itakavyowafunika wapinzani wao Sikinde.
Kiongozi wa Bendi ya Sikinde, Habib Abbas 'Jeffa' naye akielezea jinsi bendi yake itakavyofanya makamuzi siku hiyo.
Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.
Diamond Platnumz (kushoto) akiwa katika pozi na H-Baba baada ya mkutano huo.
---
Baadhi ya wasanii, wabunge na wanamasumbwi watakaoshiriki katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, leo walikusanyika katika mkutano wao na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza jijini Dar na kuelezea jinsi walivyojipanga kuelekea katika tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika Julai 7, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika tamasha hilo, wabunge wa Simba na wale wa Yanga watashuka dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya ndondi dhidi ya waigizaji. Kwenye eneo la ndondi, Mhe. Halima Mdee atapigana na Jacqueline Wolper, Mhe. Zitto Kabwe na Vincent Kigosi ‘Ray’, Mhe. Ester Bulaya atavaana na Aunt Ezekiel huku balaa zaidi likitarajia kuandikwa na mabondia Patrick Amote (Mkenya) atakayevaana na Thomas Mashali (Mtanzania) huku Mkenya Shadrack Muchanje akipigana na Francis Miyeyusho (Mtanzania). Burudani nyingine zitakazokuwepo siku hiyo ni wakali wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Prezzo, ambao watashindana katika jukwaa moja ili kutafuta nani mkali zaidi. Bendi za Msondo Ngoma, Mlimani Park ‘Sikinde’ na Jahazi zitawaburudisha mashabiki wao. Vilevile, burudani nyingine itatoka kwa wakali wa Temeke, Wanaume Family na Halisi, wataokata mapanga Taifa kwa staili zao za kuvutia. Soka la kukata na shoka kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva litahakikisha linawapa raha mashabiki wa wasanii watakaoingia uwanjani siku hiyo.

GPL

Dida aanza mazoezi Yanga, timu kuondoka Ijumaa kwenda Kanda ya Ziwa


 Mlinda Mlango Deogratius Mushi 'Dida' akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga, Loyola Sekondari hii leo.
  Na Baraka Kizuguto
KIPA mpya aliyesajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Deogratius Munishi 'Dida' pamoja beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Rajab Zahir leo wameanza rasmi mazoezi na timu yao Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema jana katika siku ya kwanza ya mazoezi kiungo mshambuliiaji Mrisho Khalfan Ngassa alifanya mazoezi asubuhi chini ya kocha mholanzi Ernest Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi wachezaji wote wa timu ya taifa, Taifa Stars kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji watano wapya ambao ni Dida kutoka Azam, Zahir wa Mtibwa, Ngassa wa Simba, Shaban Kondo aliyekuwa Msumbiji na Realitus Lusajo kutoka Machava FC.
Kocha Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji hao kwani amesema atapata fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki kanda ya ziwa hali itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na msimu mpya wa 2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi Loyola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ziara yake Kanda Ziwa inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.

Wachezaji wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu