Monday, July 22, 2013

NMB YAFADHILI SEMINA YA MAAFISA MAENDELEO WA VIJANA NCHINI

Benki ya NMB imefadhili semina kubwa iliyohusisha maafisa maendeleo wa vijana kutoka nchi nzima.Semina hii ambayo ilikua ni ya siku mbili ilifanyika katika kumbi za uwanja wa Taifa  jijini Dar es salaam. Mhe. Dkt.Fenella Mukangara ambae ni Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo  alizindua rasmi semina hii na kuishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili mkubwa ambao wamejitolea ili kufanikisha semina. Dhumuni la semina ni  kujadili maendeleo ya vijana kuanzia ngazi ya halmashauri,kuimarisha utendaji kazi kwa vijana wa mikoa na wilaya.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  akifungua semina ya Maofisa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kudhaminiwa na benki ya NMB. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo  Bw. Seth Kamuhanda akifafanua  jambo wakati wa semina hiyo.Meneja wa NMB Mikopo Midogo Midogo Bw. Mashaga Changarawe akielezea huduma mbali mbali   zitolewazo na Benki ya NMB zikiwemo akaunti pamoja na mikopo mbalimbali kwa wajasiriamaliMeneja Mawasiliano  wa NMB, Josephine Kulwa akizungumzia jinsi ambavyo Benki ya NMB kwa kupitia huduma zake kwa wajasiliamali inavyosaidia kuongeza ajira kwa vijana nchiniErick Shigongo nae alitoa maada kuhusiana  mafanikio na kujitambua katika ajira.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu