Sunday, July 21, 2013

PICHA ZA MATUKIO YA KUWASILI KWA MIILI 7 YA WANAJESHI WA JWTZ WALIOUAWA SUDAN


MKUU WA MAJESHI GENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AKISUBIRI KUPOKEA MIILI YA VIJANA WAKE WALIOUAWA SUDAN

BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI WAKIONGOZWA NA MAKAMU WA RAIS DR MOHAMMED GHARIB BILAL

MAMA SALMA KIKWETE NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NAO WALIKUWEPO


NDEGE ILIYOBEBA MIILI YA WANAJESHI MARA BAADA YA KUWASILI KUTOKA SUDAN



MIILI YA WANAJESHI 7 WALIOUAWA SUDAN IKIONEKANA KWENYE NDEGE MARA BAADA YA KUWASILI


WANAJESHI WA JWTZ WAKIBEBA MIILI YA WENZAO WALIOUAWA HUKO SUDAN

NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAKISUBIRI KUWASILI KWA MIILI YA WANAJESHI WALIOUAWA SUDAN


ILIKUWA NI VIGUMU KUVUMILIA HALI HII BAADA YA KUONA MIILI YA WAPENDWA WAO


HALI ILIKUWA YA MACHUNGU KWA NDUGU WA KARIBU

WANAJESHI WA JWTZ WAKIPOKEA MIILI YA WENZAO

MIILI IKITOLEWA KWENYE NDEGE

MMOJA KATI YA MIILI YA MAREHEMU UKIINGIZWA KWENYE GARI

MOJA KATI YA FAMILIA ZA MAREHEM WALIOUAWA SUDAN

FAMILIA ZA MAREHEM WAKISUBIRI KUWAPOKEA WAPENDWA WAO
Miili ya wanajeshi saba mashujaa wa Tanzania waliofariki wakiwa kazini wakitekeleza ulinzi wa amani wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini Sudan, imewasili leo kwa ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Kaimu Mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili hiyo imewasili leo Jumamosi majira ya saa 9.45 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.

Miili iliyowasili ni ya Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.

Shughuli za kuagwa miili ya wanajeshi hao zitafanyika katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa vilivyoko Upanga jijini Dar es salaam.

Kuwapoteza wanajeshi hawa ni la kwanza na kubwa kwa nchi ya Tanzania tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007. Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walifariki dunia mwezi uliopita baada ya chombo chao cha kusafiria kusombwa na maji ya mto uliokuwa umefurika huko nchini Sudan. 

HABARI/PICHA NA BONGOCLAN.COM
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu