Thursday, July 11, 2013

SHEREHE KUKABIDHI KOMBE LA DIWANI WA KATA YA KIPAWA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akimpa mfano wa zawadi ya hundi ya shs laki moja mfungaji bora wa mashindano hayo.



PICHA ZOTE NA MPIGA MPICHA WETU.
Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakicheza katika viwanja vya Stakishali, Segerea baada ya kumalizika kwa mashindano ya Diwani Bonnah Cup ambapo timu ya stakishari ilikuwa mabingwa.

Charles Baba Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akiimba wimbo wa risasi kidole uliokonga nyoyo za wapenzi wa muziki baada ya mashindano ya Diwani Bonnah Cup katika viwanja vya social Stakishali, Segerea kushoto ni diwani Bonnah Kaluwa.

Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonna Kaluwa akiserebuka muziki  ulikuwa ukipolomoshwa na bendi ya Mashujaa katika viwanja vya Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.

Charles Baba, Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akitumbuiza baada ya mashindani ya Diwani Bonnah Cup yaliyomalizika mwishoni mwa wiki. Anaye pga makofi ni muuandaji wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa katika viwanja vya Social Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.

Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa akifurahi kwa kucheza baada ya mashindano aliyoandaa ya Bonnah Cup yaliyoshirikisha zaidi ya timu 20, Anayeimba ni Charles Baba Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa katika viwanja vya social  Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu