Tuesday, July 2, 2013

Sio kiSio kikapu tu hata soka najua! Obama akionyesha manjonjo yake


IMEKUWA ikifahamika kuwa Rais wa Marekani Barack Obama ni mahiri katika mpira wa Kikapu na ndoto zake ilikuwa aje kucheza Ligi maarufu ya mchezao huo nchini mwake, NBA kabla ya upepo wa siasa haujamvuta na kumpeleka kuweka historia ya kuwa Rais wa kwanza mweusi nchini humo.
Hata hivyo kumbe sio kikapu tu hata soka analijua vyema kama pichani anavyoonekana akionyesha manjonjo yake mbele ya mwenyeji wake Rais Jakaye Kikwete ambaye naye ni mnazi mkubwa wa mchezop humo nchini na michezo kwa ujumla.
Rais Kikwete akimwangalia Obama wakati akipiga mpira danadana.OBAMA akionyesha uwezo wa kumiliki mpira kwa kupiga kichwa bila kutua chini wakati alipotembelea mitambo ya kufua umeme Ubungo jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuondoka nchini.Hapa akipiga danadana huku akishuhudiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu