Zantel yamleta mkali wa Azonto Dar es Salaam
- Kutoa burudani kali viwanja vya Posta kesho
Mwanamuziki huyo
ambaye anatamba na wimbo wake wa Azonto, analetwa kwa ushirikiano wa kampuni ya
simu za mikononi ya Zantel, pamoja na Times FM.
Burudani hiyo
inatarajiwa itaanza kuanzia mida ya saa mbili usiku hadi majogoo kwa kiingilio
cha shilingi elfu kumi kwa kununua tiketi kabla na elfu kumi na tano kwa
watakao nunua tiketi mlangoni.
Akimzunguzia mkali
huyo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema Zantel imemleta msanii
huyo ili kuwapa ari wasanii wa ndani wenye lengo la kufikisha kazi zao hatua za
kimataifa.
‘Zantel imekuwa
msitari wa mbele katika kuwawezesha wasanii wa ndani, hasa vijana, na kwa
kumleta Fuse ODG, ambaye ni mmoja wa wasanii wachache kutoka Afrika
waliofanikiwa kufikisha mziki wao soko la kimataifa tunaamini vijana
watajifunza mengi’ alisema Khan.
Fuse ODG ni
mwanamuziki wa Ghana mwenye makazi nchini Uingereza, ambaye wimbo wake wa
Azonto ulifanikiwa kuwa namba moja kwenye iTunes World Chart, akiwa ni
mwanamuziki wa kwanza kutoka Ghana kufikia mafanikio hayo.
Kwa wimbo wa Azonto
pekee, Fuse ODG alifanikiwa kupata watazamaji zaidi ya milioni kumi na moja
kwenye You Tube kwa mwaka 2012.
Naye Mkurugenzi wa
Times FM, Rehure Nyaulawa, alisema wamemleta msanii huyo ili kuhakikisha
watanzania wanapata burudani wanayoipenda ya Azonto hapa hapa nchini.
‘Azonto imejipatia
umaarufu mkubwa karibu dunia nzima, lakini pia kwa upande wa radio yetu wimbo
huu umepata maombi mengi kuliko wimbo wowote wa kimataifa kiasi cha kuona
tuwaletee watanzania burudani wanayoipenda’ alisema Nyaulawa.
Fuse ODG
atasindikizwa na wasanii wote wa kundi la BHitz, Mshindi wa Epiq BSS Walter
Chillambo, Menina pamoja na wasanii wa Marco Chali Foundation.
Wimbo wake mpya wa
Antena ambao amemshirkisha Wyclef Jean unafanya vizuri kwenye chati mbalimbali
duniani kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment