Saturday, September 21, 2013

Simba, Mbeya City uso kwa uso, Mtibwa yaifuata Prisons Mbeya, kivumbi za FDL nacho mmh! yanga kesho

Mbeya City
Simba
Na Boniface Wambura

BAADA ya kuifanyia mauaji ya kutisha Mgambo JKT, vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba kesho itaikaribisha Mbeya City ambayo iliyozidindia Yanga na Mtibwa Sugar katika mechi zake mbili zilizopita.
Simba itaialika Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu kwenye dimba la Taifa ikiwa ni muendelezo ya michezo ya ligi kuu (VPL) inayopingia raundi yake ya tano ambapo pia itashuhudiwa michezo mingine mitatu tofauti.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.


Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.


Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.


Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).


Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. 
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.


Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. 
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu