Monday, September 2, 2013

Wabongo wawili waombewa ITC Ujerumani



Na Boniface Wambura
CHAMA cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.

Maombi hayo yaliyotumwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kwa ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba 31, 1984 jijini Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14, 1991 jijini Tanga.

Wachezaji hao wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito anaombewa hati hiyo ili ajiunge na klabu ya FSV Lokomotive Dresden wakati Johnson anatakiwa na klabu na TSV 1967 Schwabbruck.


Usaili wa wagombea TFF, Bodi ya Ligi kukamilika leo

Na Boniface Wambura
USAILI wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na unatarajia kukamilika leo (Septemba 1 mwaka huu).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni ilianza usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa kutangazwa keshokutwa (Septemba 3 mwaka huu).

Kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati hiyo.

Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya maadili. Kwa watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufani kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6 mwaka huu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu