wakati wa uokoaji unaendelea kwa kasi mpaka hivi sasa Iadadi za maiti zilizopatikana ni 28 kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia tutazidi kuwaletea habari zaidi endelea kuangalia blog yenu
Home » Archives for March 2013
Sunday, March 31, 2013
SHEREHE YA PASAKA LEO
MHASHAMU Askofu wa kanisa Katoriki jimbo la Morogoro Telesphori Mkude,akihutubia mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada pasaka ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Patriki Mjini Morogoro,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 28 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Baadhi ya watu mbalimbali waliofika katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa aajili ya kutambua ndugu zao waliokufa kwa ajali ya kuangukiwa na ghorofa
Baadhi ya waumini wa kanisa la St Joseph jijini Dar es salaam wakitoka katika ibada ya Pasaka leo
Muuguzi mkunga Fatuma Uwesu wa Hospitali ya Mwananyamalakulia akimpa chanjo mtoto ambaye aliezaliwa katika mkesha wa pasaka kushoto ni mama wa mtoto huyo Maria Weus leo
Masita wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma wakisikiliza mahubiri ya Askofu Gervas Nyaisonga jana katika kanisa la Mt Paulo wa Msalaba Dodoma mjini
Askofu mkuu wa kanisa la Injili la KKKT Dr Alex Malasusa akimbariki mtoto wakati wa ibada ya Pasaka leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwasili katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kuwajulia hali vijana Mohamed Ally Dhamji (kushoto), Baqir Virani, ambaio ni kati ya majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 28 mpa leo
Baadhi ya waumini wa kikristo wa kanisa la kkkt la Azania wakielekea katika kutoa sadaka wakati wa ibada ya Pasaka leo
Saturday, March 30, 2013
AJALI YA GHOROFA LILILOANGUKA IDADI NI 20 WALIOKUFA
JUMUIYA WAISLAM WATOA DAMU KUWASAIDIA WAGONJWA
Jumuia ya Waislam kitengo cha Afya na Ustawi wa jamii (Jumuiyatul-Akhalaaqul=Islaam (JAI) Taasisi isiyo ya kiserikali leo walijitolea Damu ili kuwasaidia wagonjwa wa jinsia zote madhehebu zote na imani zote na wagonjwa walio mawodini na majumbani Taasisi hiyo ilitoa damu katika kitengo cha Damu salaama kilichopo Muhimbili
picha imuonyesha mhudumu wa kitengo cha damu salaam Mariam Kabona akimtoa damu Dk Nassir Rajabu Khamisi leo
picha imuonyesha mhudumu wa kitengo cha damu salaam Mariam Kabona akimtoa damu Dk Nassir Rajabu Khamisi leo
BREKING NEWZZZZZZZZZZZ
Katika ukoaji unaondelea kwenye jengo lililoanguka jana jumla ya maiti nane 8 zimepatikana kwa mujibu ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick huku juhudi zinaendelea na kuongezea nguvu na vifaa mbalimbali vilivyongezwa tutaendelea kukufahamisheni kadri inapotokea usikose
Friday, March 29, 2013
RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA JENGO LILILOANGUKA LEO
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisindikiwa na Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova baada ya kutembelea eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
PICHA NA IKULU
KUAGA MWILI WA ALIEKUWA MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED KHAMIS LEO
Rais
Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine
wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis,
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF,
aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za
kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka
kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga
mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba,
Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Rais
Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge) William Lukuvi, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,
Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki
shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki
jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji
wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF,
aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye
gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa
maziko, yatakayofanyika leo.
*BREAKING NEEEWZ!!! JENGO LA GHOROFA 14 LAPOROMOKA DAR LAFUKIA WATU KADHAA
Friday, March 29, 2013
No comments
Jengo
la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa
Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na
kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi
haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha
katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka
leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama
'Tetemeko la ardhi'.
Aidha
imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa
wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza
chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza
kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote
inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji
wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali
yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Waokoaji wakiwa hoi......
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.
MAITI ZAIDI YA 10 NA MAJERUHI 30 TU WACHOMOLEWA HADI SASA KATIKA MABAKI YA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI HII NA KUWAFUNIKA WATU KIBAO WAKIWAMO MAFUNDI WALIOKUWA WAKIENDELEA KULIJENGA... NI JIRANI NA MSIKITI WA SHIA MAKUTANO YA MOROGORO ROAD NA INDIRA GANDHI... HARAKATI ZA KUCHOMOA MAJERUHI NA MAITI ZAIDI ZINAENDELEA ZIKIONGOZWA NA VIONGOZI KADHAA WA SERIKALI AKIWAMO RC DAR, SAID MECK SADICK
Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka asubuhi hii katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 29, 2013. |
Tukio hilo limetokea mishale ya asubuhi katika mitaa ya Posta, jirani na msikiti wa Shia katika eneo la makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi na hadi sasa, miili ya maiti 12 na pia majeruhi 30 wameshachomolewa.
Aidha, harakati zaidi za uokoaji zingali zikiendelea kufanywa na vikosi vya uokoaji. Katika eneo la tukio hilo, tayari viongozi kadhaa wa serikali na makamanda wa Polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam wamefika kusaidia shughuli za uokoaji, miongoni mwao akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa mabaki ya jengo hilo yanaonyesha kuwa mchanga ulikuwa mwingi mno kulinganisha na saruji, hali inayodhaniwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa mjengo huo uliogharimu mamilioni ya pesa.
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi za serikali zilizotolewa kuelezea msiba huo
BREAKING NEWS; JENGO LA GHOROFA 16 LAANGUKA KATIKATI YA JIJI
Changamoto ya
uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo,
ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
Hizi nia aina
ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa
ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za
ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.
Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.
Waziri wa
Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka
kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova
kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi
katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha
Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote
na Habari Mseto Blog)
Waokoaji wakiwa kazini.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.
Subscribe to:
Posts (Atom)