Tuesday, April 30, 2013

MATUKIO TA MVUA

0 comments

Polisi wa usalama barabarani akimueleza dereva wa daladala kuhusu uendeshaji mbaya wa kutanua pembeni mwa barabara eneo la makumbushoa barabara ya Ali hassan Mwinyi leo 

MVUA ZINAZOENDELEA HIVI SASA ZIMESABABISHA BARABARA KUJAA MAJI KAMA INAVYONYESHA LEO 


Mamam huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa anatoa maji kati nyumba yake eneo la mwananyamala kwa kopa leo kutokana na mvua 

jiji la Dar es salaam limenogeshwa kwa mambo mbalimbali mzunguko wa makutano ya barabara ya msimbazi na uhuru picha kubwa ngalawa na mchoro wa bahari 
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakisubiriana kupita katika mawe yaliyowekwa kutokana na dimbwi la maji ili wapate kudanda kama picha hii inavyonyesha leo kariakoo dsm
Endelea Kusoma >>

MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI

0 comments

LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA 25

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi.



Licha ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013), mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu nchini.



Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa.



Viingilio katik mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.



Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.



Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons. Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.







MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.



Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.



Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.



MECHI YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/-

Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.



Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.



Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.



Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>

Monday, April 29, 2013

0 comments

AZAM WATUA RABAT WAMECHOKA ILE MBAYA KWA UREFU WA SAFARI

Kocha wa Azam FC, Stewart Hall akizungumza na Florian Kaijage Mratibu wa klabu katika mashindano ya Afrika, baada ya kuwasili Cassablanca leo

Na Mahmoud Zubeiry, Rabat
AZAM FC imewasili salama nchinio Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji, FAR Rabat, Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii.  
Azam, imewasili Cassablanca, majira ya saa 9:15 za huku Alasiri, sawa na saa 10:15 za Afrika Mashariki na kusafiri kwa basi kwa saa mbili kwenda Rabat, mji ambao mechi itachezwa.
Azam imetua Morocco ikitokea Dubai, UAE ambako ilifika usiku jana saa 6:00 kwa saa za huko sawa na saa 5:00 kwa saa za Afrika Mashariki, ikitokea Dar es Salaam.
Msafara huo unaouhusisha wachezaji na benchi la Ufundi, baada ya awali viongozi na wapenzi kadhaa kutangulia nchini humo, ili kuweka mazingira sawa, uliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la Emirates, wadhamini wa Arsenal ya England saa 11:00 jioni kwa saa za Tanzania.
Ni safari ndefu iliyohusisha mabara mawili, kutoka Afrika, Tanzania kupitia Asia Dubai na kurudi Afrika nchini Morocco.
Azam walilala katika hoteli ya nyota tano ya Copthorne Dubai kabla ya kuunganisha ndege saa 7:35 asubuhi ya leo kuja Morocco kesho.
Wachezaji wanawasili Morocco

Azam imefikia katika hoteli ya Golden Tulip, maeneo ya Rabat, kaskazini mwa Cassablanca,  kilomita 120 kutoka Uwanja wa Ndege wa Cassablanca, umbali wa takriban saaa mbili.
Azam itaanza rasmi mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo, ambao wanatakiwa kutoa sare ya mabao au kushinda ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Japokuwa hilo linachukuliwa kama jambo gumu mbele ya wengi, lakini rekodi ya timu hiyo, mali ya bilionea Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inaonyesha linawezekana.
Wachezaji wanatua Morocco

Azam imekuwa ikicheza vizuri na kupata matokeo mazuri katika mechi za ugenini kwenye michuano hii, kuliko nyumbani na hata kufuzu kwake hadi hatua hii zaidi kulitokana na matokeo ya mechi za ugenini.
Raundi ya kwanza, Azam ilianza kwa kushinda kwa taabu 3-1 Dar es Salaam dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini, sehemu kubwa ya mchezo huo matokeo yakiwa 1-1 kabla ya mabao ya dakika za jioni ya Kipre Tchetche kutengeneza ushindi huo.
Mchezo wa marudiano, Azam ilishinda 5-0 ugenini na kufanya ushindi wa jumla wa 8-1, ikisonga mbele kibabe.
Raundi ya Pili, ilianza kwa ushindi wa 2-1 ugenini, Liberia dhidi ya wenyeji, Barack Young Controllers II, lakini katika mchezo wa marudiano ilibanwa kwa sare ya 0-0.
Kocha Muingereza Stewart Hall hakuipa umuhimu mechi ya Ligi Kuu Ijumaa dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga iliyoisha kwa sare ya 1-1 akiwapumzisha wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi na FAR Rabat.
Wakati mabeki Waziri Salum, Joackins Atudo, viungo Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Balou na mshambuliaji Kipre Tchetche hawakukanyaga kabisa nyasi za Uwanja wa Mkwakwani Ijumaa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alicheza kwa dakika 15 tu za mwisho- ili kuhakikisha wanakuwa vizuri Jumapili mjini Rabat.
Kutoka kikosi cha kwanza cha sasa cha Azam waliocheza dakika zote juzi ni kipa Mwadini Ally, kiungo aliyehamishiwa beki ya kulia, Himid Mao, beki David Mwantika, kiungo Humphrey Mieno na washambuliaji Brian Umony na John Bocco ‘Adebayor’.
Azam, itakuwa Rabat kwa wiki nzima hadi Jumamosi itakapocheza mechi na imejipanga vema kuhakikisha inavuka hatua hii
Endelea Kusoma >>
0 comments

HATIMAYE LEMA AACHIWA NJE KWA DHAMANA ASEMA POPOTE MKUU WA MKOA ATAKAPO ONEKANA AZOMEWE


Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mbunge wa Arumeru Mashariki katika msafara mara baada ya mmbunge wa Arusha mjini aliyefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kusababisha fujo na kumkashifu mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo  kuachiwa huru kwa dhamana
Endelea Kusoma >>

MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA ACHIWA KWA DHAMANA LEO

0 comments

Wafuasi wa chama cha Maendeleo na Demokrasia Chadema wakiwa katika msafara mkubwa wakinsindikiza mbunge wa jimbo la Arusha mjini  Godbless Lema akiwa
na mbunge wa jimbu la Arumeru mashariki wakiwa juu ya gari wakitokea mahakamani  mara
baada ya kuachiwa huru kwa dhamana  baada ya kukamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi
 kwa muda wa siku tatu kwa madai ya kuchochea wanafunzi wa chuo kufanya ghasia
Endelea Kusoma >>

Sunday, April 28, 2013

0 comments


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuomboleza kifo cha Mjumbe wa Baraza la Seneti na Waziri muhimu wa zamani wa nchi hiyo, Mheshimiwa Mutula Kilonzo, aliyefariki dunia juzi, Ijumaa, mjini Nairobi.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amemwambia Rais Kenyatta kuwa amepokea habari za kifo cha ghafla cha mwanasiasa huyo kwa mshtuko na huzuni na kuwa kifo chake kimeipokonya nchi hiyo mmoja wa viongozi waliokuwa wanajali na kutanguliza maslahi ya Kenya na wananchi wake.
“Kwa hakika, kifo cha Mheshimiwa Mutula Kilonzo kimeipokonya Kenya kiongozi muhimu. Mchango mkubwa aliuotoa katika kipindi cha kuivusha Kenya kutoka kwenye changamoto za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 hadi sasa ambako nchi imetulia na inasonga mbele, kamwe hautasahaulika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika nafasi zote za Uwaziri alizozishikilia katika kipindi hicho, kwanza kama Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba na baadaye kama Waziri wa Elimu, alijithibitisha na kujipambanua kama Mzalendo wa kweli kweli wa Kenya na mpenzi halisi wa nchi yake.”
Ameongeza Rais: “Nakutumia Mheshimiwa Rais salamu zangu za rambirambi na zile za Serikali yangu kufuatia msiba huu. Aidha, kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu kwa familia ya Mheshimiwa Kilonzo. Nataka wajue kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na naungana nao kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mutula Kilonzo.Amin.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
Endelea Kusoma >>
0 comments

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo mchan. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa ufunguzi wa kikao cha juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofaniyka jijini Arusha.
 Marais  Wa jumuiya ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano wa Wakuu wa jumuiya hiyo katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo.Kutoka kushoto ni Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi,Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Mwenyeji wa mkutano Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mpya wa Kenya,Uhuru Kenyatta(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi bbada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha(picha na Freddy Maro)

Rais .Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowasili juzi jioni kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki unaofanyika jijini Arusha. (PICHA NA FREDDY MARO)
Endelea Kusoma >>

KOMBE LA SAFARI LAGER

0 comments
  - Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akipokea Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager kutoka kwa Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo ikiwa ni kutoa Baraka zake kwa Kombe hilo kuwepo jijini Mwanza,katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo.



 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akinyanyua Juu Kombe la Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager wakati wa kutoa baraka zake kwa ziara ya Kombe hilo jijini Mwanza.

Endelea Kusoma >>

EXTRA BONGO YAZIDI KUWABAMBA MASHABIKI NDANI YA MEEDA SINZA

0 comments


Mkurugenzi wa Extra bongo Ally Choki akiimba mbele ya mashabiki wake (Hawapo Pichani) ndani ya Ukumbi wa Meeda sinza jana Usiku wakati bendi yake ilipokuwa ikiburudisha pande pande hizo
Kushoto ni mwimbaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo Athanas akiwa na Mwimbaji pekee wa kike wa bendi hiyo Khadija Mnoga a.k.a "Kimobitel" ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake wa "Mgeni" wakishoo luv mbele ya kamera yetu ndani ya ukumbi wa Meeda Sinza jana usiku wakati Bendi yao ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo.
Kushoto ni mmoja wa marapa bora wa muziki wa dansi Totoo Ze Bingwa akirap ndani ya Meeda sinza wakati Bendi anayopigia mzigo Extra Bongo ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo na kulia ni Banza Stone a.k.a Generale akimpa big up.
Maua ya Extra Bongo mzigoni
Wakata nyonga maarufu kwa sasa wa Extra bongo wakiongozwa na nyamwela wakiwapagawisha mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Meeda Sinza jana usiku
Waimbji bora wa Extra bongo kulia ni Rogert Hega a.k.a Katapila wakiimba ndani ya Meeda Sinza jana usiku
Rapa bora wa Extra bongo Kabatano (Kulia) akigani moja ya jimbo zao bora huku akipewa sapoti na nguli wa muziki wa dansi Banza Stone mwana masanja wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza maeneo ya Sinza katika ukumbi wa Meeda jana usiku
Endelea Kusoma >>

Saturday, April 27, 2013

0 comments

WASHIRIKI WA MISS MANISPAA YA ILEMELA WATEMBELDEA KIWANDA CHA COCA-COLA JIJINI MWANZA


 Washiriki wa Shindano la Miss wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza 2013, wakifurahia jambo na mwandaaji wa shindano hilo, Restuta Mushi (aliyechuchumaa), wakiwa katika kiwanda cha Coca Cola jijini Mwanza, (Picha na Sitta Tumma).
Washiriki wa Shindano la Miss wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza 2013, wakiwa katika pozi la pamoja muda mfupi baada ya kuzuru kwenye kiwanda cha Coca Cola jijini Mwanza, juzi
Endelea Kusoma >>
0 comments

YANGA SC WAANZA MCHAKATO WA KULIPA 5-0 ZA MNYAMA, WAINGIA GYM LA KISASA QUALITY CENTRE KUTANUA VIFUA

Wachezaji wa Yanga SCwakiwa mazoezini kwenye gym ya Quality Centre, Dar es Salaam asubuhi ya leo kujiandaa na mechi mbili zilizobaki za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  Yanga tayari wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu na sasa wanacheza kukamilisha ratiba, wakiwa wamepania kushinda mechi zote na zaidi kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 na wapinzani wao wa jadi, Simba SC Mei 18, baada ya kucheza na Coastal Union Mei 1, mwaka huu. 

Kevin Yondan...

Haruna Niyonzima na Hamisi Kiiza...

Oscar Joshua...

Kevin Yondan...

Said Bahanuzi na Mbuyu Twite...

Meneja Hafidh Saleh
Endelea Kusoma >>

ANITHA ATWAA TAJI LA MISS ELIMU YA JUU MORO 2013

0 comments


Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na mshindi wa tatu, Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Tarchisic Mtui, akijinadi mbele ya majaji na kivazi cha ubunifu alichokitengeneza kwa majani ya mti, Muashock wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu mkoani humo.
Washiriki wa shindano la  Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange, akijinadi mbele ya majaji na kivazi cha ufukweni wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Hellen Mhando akipita jukwaani kujinadi mbele ya majaji na kivazi cha usiku wakati wa  Shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya kutwajwa wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce,Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ‘Bongo Fleva’ Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia ya urembo wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakati wa wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.
Endelea Kusoma >>

Thursday, April 25, 2013

REAL MADRID KAMA BACELONA YACHEZEA KICHAPO 4-1 NA DORTMUND, MOURINHO HOI

0 comments

 MABAO manne ya Robert Lewandowski usiku huu yameipa Borussia Dortmund ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.

Mabao hayo ya mshambuliaji huyo wa Poland yanawafanya Dortmund watengeneze mazingira ya fainali ya klabu za Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini mshambuliaji huyo akarudi na makali zaidi kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo leo, sasa anatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.
Kikosi cha Borussia Dortmund kilikuwa: Weidenfeller, Piszczek/Grosskreutz dk83, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan/Schieber dk90, Blaszczykowski/Kehl dk82, Gotze, Reus na Lewandowski.
Real Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso/Kaka dk80, Ozil, Modric/Di Maria dk68, Ronaldo na Higuain/Benzema dk68.
On fire: Robert Lewandowski scored all four goals as Dortmund crushed Real Madrid in their semi-final first leg
Moto: Robert Lewandowski amefunga mabao yote manne ya Dortmund dhidi ya Real Madrid leo
Perfect start: Lewandowski put Dortmund ahead as early as the eighth minute
La kwanza: Lewandowski akiifungia Dortmund bao la kwanza
Lead: Lewandowski peeled away at the far post to guide Mario Gotze's cross into the far corner
Lewandowski Robert Lewandowski AKISHANGILIA BAO
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
La kusawazisha: Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
Ahead again: Lewandowski held off Raphael Varane's challenge to give the Germans a 2-1 lead
La pili: Lewandowski akifunga la pili
Lewandowski
Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu