Home » Archives for July 2013
Wednesday, July 31, 2013
NEYMAR, MESSI WAANZA KAZI PAMOJA BARCA...PACHA JIPYA LA HATARI LA USHAMBULIAJI DUINA NZIMA
MCHEZAJI mpya wa Barcelona, Neymar ameanza mazoezi na timu yake hiyo mpya baada ya kukamilisha vipimo vya afya.
Wachezaji wote wa Barcelona waliokuwa
kwenye Kombe la Mabara walitipoti jana baada ya mapumziko na Neymar
alikuwa miongoni mwao pamoja na Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas na
Lionel Messi.
Ilikuwa mara ya kwanza kukutana na
wachezaji wenzake wapya, baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili
ghali katika historia ya klabu baada ya Zlatan Ibrahimovic mwaka 2009
kusajiliwa kwa Pauni Milioni 56.
VIDEO Mazoezi ya Barcelona na wachezaji kupimwa afya jana
Si mbaya: Lionel Messi (kushoto) na Neymar (kulia) wakifanya mazoezi pamoja kwa mara ya kwanza
Neymar (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Barcelona
Neymar na mchezaji anayetakiwa na Manchester United, Cesc Fabregas (kushoto) wote walikuwa kivutio mazoezini
Nyumbani: Neymar na mchezaji mwenzake wa Brazil, Daniel Alves katika mazoezi ya Barcelona
Karibu: Kipa Victor Valdes akisalimiana na kocha mpya, Gerardo Martino
RAIS JAKAYA KIKWETE NA MGENI WAKEWaziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra leo, wameshuhudia utiaji sai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck
Shinawatra leo, Jumanne, Julai 30, 2013 wameshuhudia utiaji saini mikataba
minne ya kuimarisha ushirikiano na uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Viongozi hao wawili wameshuhudia
utiaji saini huo katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam mchana
wa leo ikiwa sehemu ya shughuli za Mheshimiwa Shinawatra katika Tanzania wakati
wa ziara yake ya siku tatu nchini.
Mikataba ambayo viongozi hao
wameshuhudiwa ikitiwa saini ni pamoja na ule wa kubadilisha wafungwa uliotiwa
na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Silima Pereira kwa niaba
ya Tanzania na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand,
Mheshimiwa Surapong Tovichachakul,.
Mikataba mingine ni mkataba wa Kuimarisha
na Kulinda Uwekezaji (Promotion and
Protection of Investments) na mkabata wa Ushirikiano katika Masuala ya
Ufundi iliyotiwa saini na Mheshimiwa Tovichachakul na Waziri wa Fedha wa
Tanzania, Mheshimiwa William Mgimwa.
Mkataba wa nne kutiwa saini ni
Makubaliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Chuo cha Madini cha Thailand
kwa niaba ya Wizara ya Biashara ya Thailand uliotiwa saini na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Madini Bwana Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Madini cha
Thailand Bi. Prom Sawatwatthanakul.
Mapema leo Waziri Mkuu wa Thailand
ambaye aliwasli nchini akitokea Mozambique katika ziara yake ya nchi tatu za
Afrika amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
na pia akalakiwa Ikulu, Dar Es Salaam na mwenyeji wake Rais Kikwete.
Viongozi hao wamekutana na kufanya
mazungumzo ya faragha na baadaye kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya
Sserikali hizo mbili.
Kubwa ambalo limekubaliwa katika
mazungumzo hayo ni umuhimu wa nchi hizi mbili kuimarisha uhusiano na
ushirikiano kati yao kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Thailand.
Baadaye viongozi hao wawili wamekwenda
kwenye Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro mjini Dar Es Salaam ambako
Mheshimiwa Shinawatra ametangaza Mpango Mpya wa Ushirikiano kati ya Afrika na
Thailand.
Mama huyo ameuambia mkutano huo wa
maofisa wa Serikali, wafanyabiashara wa sekta binafsi, wasomi, mabalozi na
wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali kuwa
Mpango huo una misingi yake katika ushirikiano wa Nchi Zinazoendelea za Kusini (South-South Cooperation).
Chini ya Mpango huo, Thailand
itaitisha mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Afrika na Thailand mwanzoni mwa
mwaka ujao na amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria mkutano huo wenye nia ya
kujenga mahusiano ya karibu zaidi kati ya Afrika na Thailand.
“Kwa kutilia maanani usawa wa ujuzi wa
jitihada za maendeleo nchi za Afrika na Thailand, nchi yangu itaongeza kasi ya
mahusiano ya maendeleo na Afrika katika maeneo ambako uhusiano huo unaweza
kuongeza faida kwa pande zote mbili, kwa jamii zetu na watu wetu hasa katika
sekta za kilimo, afya, elimu na maendeleo ya watu kwa jumla.”
Ameongeza mama huyo: “Wakati
huo huo, Thailand inatangaza leo kuanzishwa kwa Mpango wa Wanathailand
Kujitolea ambako wataalam wa Thailand watafanya kazi na wenzao wa Afrika katika
nchi za Afrika kwenye miradi iliyoko chini ya ushirikiano wa kiufundi.”
Baadaye leo, Waziri Mkuu Shinawatra
atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo imeandaliwa kwa heshima yake na Rais
Kikwete na itakayofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
Kesho,
Waziri Mkuu huyo atakwenda kwenye Mbunga ya Taifa ya Serengeti ambako atakutana
na maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watakaomwelezea hali halisi,
changamoto na umuhimu wa kulinda mbunga za wanyama. Aidha, akiwa Serengeti,
mama huyo atashuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Kushirikiana Katika
Kulinda Hifadhi na Wanyamapori kati ya Serikali za Tanzania na Thailand, ikiwa
ni pamoja na kushirikiana katika kupambana dhidi ya ujangili.
Mama huyo atarejea Dar Es Salaam
keshokutwa kumalizia ziara yake na kuondoka kurejea nyumbani.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
30
Julai, 2013
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa.
Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30 |
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu |
Tuesday, July 30, 2013
Monday, July 29, 2013
Sunday, July 28, 2013
COAST UNION YAITUNGUA SIMBA BAO 1-0 BILA MAJIBU LEO MKWAKWANI TANGA
KIKOSI CHA COAST UNION |
TIMU ya soka ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kuvitisha vigogo vya soka nchini ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 baada ya jioni hii kuizima mdomo Simba na kushinwdwa kunguruma baada ya kunyukwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki.
Pambano la leo lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga ilishuhudiwa hadi wakati wa mapumziko kukiwa hakuna mbabe yeyote baada ya timu zote kutoshana nguvu ya kutofungana.,
Hata hivyo katika kipindi cha pili Coastal walionyesha ilivyopania msimu ujao kwa kuwakimbiza Simba na kujipatia bao pekee lililowekwa kimiani na mchezaji wao mpya toka Kenya, Crispian Odula Odwenye aliyefunga katika dakika 54.
Hicho ni kipigo kingine kwa Simba katika mechi zake za karibu za kirafiki za kujipima nguvu na inamfanya kocha wake, King Abdallah Kibadeni kurekebisha mapema kikosi chake kabla ya ligi.
BOMOABOMOA IMEWAKUMBA WAKAZI WA BOKO LEO
kijiko kikiwa kazini leo kusafisha barabara |
zahanati ya boko nayo yavunjwa |
vijana nao wajipatia kuni mara baada ya kungolewa kwa miti |
mkutano wa wananchi wa boko leo |
mkutano wa wakazi leo |
wakazi wakichangia kwenye mkutanoleo |
BIBI Hamida kilemba mkazi wa boko akionyesha alama aliyowekewa na dasawa kluashiria kubomo sehemu hiyo |
moja ya jengo la ghorofa la bwana Allan Lema linatakiwa kubomolewa kupisha ujenzi wa bomba kuu lwa dawasa |
Subscribe to:
Posts (Atom)