Wednesday, December 17, 2014



Jengo la ghorofa tano limeanguka katika mji mkuu wa kenya, Nairobi Jumatano alfajiri na kusababisha kifo cha mtu mmoja na  inasadikiwa takriban familia 30 zimekwama kwenye vifusi vya jengo hilo.
Kwa mujibu wa  mwandishi wetu wa Nairobi, jengo hilo  lipo katika eneo la kaloleni  karibu na uwanja wa michezo wa city stadium. Juhudi za uokozi zinaendelea kufanyika ili kuwaokoa watu waliokwama ndani ya vifusi. 
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation  jengo hilo  ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa lilikuwa na wakazi ambao walikuwa wakiishi katika ghorofa ya chini, ya kwanza na  ya pili wakati ghorofa nyingine tatu  za juu zikiwa zinaendelea kujengwa.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu