Friday, January 31, 2014

0 comments

KINANA,MANGULA WAWASILI MBEYA KWA MAADHIMSHO YA MIAKA 37 YA CCM

 Makamu Mwenyekiti wa CCM,Phillip Mangula akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya , tayari akwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya Jumapili Februari 2. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Mangula (katikati) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akizungumza na Nape (kulia) pamoja na Zambi kwenye chumba cha watu mashuhuri (VIP) alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya leo mchana, ttayari kwa maadhimidho hayo.
 Nape (kulia) akizungumza na Kinana pamoja na Zambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe
Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Dogo Idd Mabrouk wakati wa mapokezi hayo.Picha na MichuziJr wa Michuzi Media Group.
Endelea Kusoma >>
0 comments

SUPER D AMPONGEZA BONDIA MUSSA MCHOMANGA NA KUMZAWADIA

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu 

Bondia Anton Idoa akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mussa mchopanga wakati wa mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Mchopanga alishinda raundi ya pili 

Bondia Anton Idoa kushoto akirusha konde ambalo alijareta madhala kwa mpinzani wake ambae anamwangalia Mussa Mchopanga wakati wa Mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya pili 


Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwinua mkono juu bondia Mussa Mchopanga baada ya kumvalisha medali ya Dhaabu baada ya kuibuka mshindi wa mkoa wa Dar es salaam 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu 



Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam 

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya dhaabu bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam 

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya Fedha bondia Abdul Rashidi  mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Endelea Kusoma >>

Thursday, January 30, 2014

0 comments



WAZIRI MSTAAFU SAMUEL MALECELA AKIONYESHA FULANA ILIYOANDIKWA JINA LA LOWASSA
  john minja
        Today at 4:54 PM

To

        samuel shelukindo
        Naimi Aziz
        Begum Taj

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014



Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.


JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Endelea Kusoma >>
0 comments

Mbwana Samatta Mchezaji Bora wa TP Mazembe 2013


Samatta akiokota mpira nyavuni baada ya kutupia
MSHAMBULIAJI Nyota wa Kimataifa wa Tanzania anayeichezea TP Mazembe, Mbwana Samata, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2013 wa klabu hiyo ya DR Congo.
Mbwana alipata kura nyingi zaidi, kuwashinda wenzake, ambao kwa mujibu wa tovuti ya TP Mazembe, yeye alipata pointi 248, huku nafasi ya pili ikishikwa na Asante Solomon aliepata kura 219.
Ulikuwa ni mwaka wa mafanikio pia kwake, pia akiwa na kumbukumbu ya kutajwa kati ya wachezaji ambao wanawania tuzo za Wachezaji wanaocheza barani Afrika, nakuchujwa baadae.
Zaidi ya hiyo, ameisaidia timu yake ya TP Mazembe katika michuano ya ndani na kimataifa, bila kusahau msaada pia aliuutoa kwa timu yake ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Endelea Kusoma >>
0 comments

Mhe. Temba, Cassim Mganga wana Lavalava la pamoja

Mhe Temba

Cassim Mganga

WASANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Mheshimiwa Temba na Cassim wanatarajia kuachia hadharani kazi yao mpya ya pamoja iitwayo 'Lavalava' Ijumaa wiki hii.
Akizungumza na MZUKA WA FUNGO meneja wa wasanii hao Said Fella, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio za Burn Records chini ya prodyuza Sheddy Clever.
Fella alisema 'kolabo' hiyo ni mwanzo tu kwa wasanii hao kutoka TMK Wanaume Family na ukoo wa Tip Top Connections kufanya kazi kwa pamoja ikiwamo kuja kuzalisha albamu kamili.
"Katika kuendelea udugu baina ya wasanii mbalimbali nchini, Mhe. Temba na Cassim Mganga wametengeneza wimbo wa pamoja uitwao 'Lavalava' na utaachiwa hewani kuanzia Ijumaa ijayo na kama mambo yakienda vyema wasanii hao wanaweza kuja kutoa albamu ya pamoja," alisema Fella.
Cassim anayefahamika kama 'Tajiri wa Mapenzi' anatamba kwa sasa na wimbo wake uitwao  I Love You', huku Mhe Tamba anakimbiza kupitia kibao chake kiitwacho 'Toroka Uje' alichoimba na Dogo Aslay na akiwa mbioni kuachia dokomentari yake iitwayo 'Maskini Jeuri'.



Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu