Home » Archives for June 2014
Monday, June 30, 2014
WAZIRI MKUU: MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA YANAENDELEA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu yanaendelea japo kwa kiasi kikubwa hatma yake inategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Juni 30, 2014) wakati akizungumza na Mameya wa Majiji, Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya Tanzania katika kikao cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga.
Waziri Mkuu yuko Tanga kwa ajili ya sherehe za Serikali za Mitaa ambayo kilele chake kitafanyika kesho Julai mosi kwenye uwanja wa Tangamano jijini hapa. Ameamua kukutana na viongozi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kukutana nao aliyoitoa Mei 14, 2014 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa ALAT.
"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni kitendawili kwa sababu kwa kiasi kikubwa inategemea sana kukamilika kwa Mchakato wa Bunge la Katiba," alisema na kuongeza:
"Kama Wizara tunaendelea na maandalizi tukiamini uchaguzi upo, kama hiyo fursa isipotokea bado tutakuwa tumekamilisha maandalizi kwa upande wetu.Tunaendelea kuandaa kanuni kwa kushirikisha wadau wote," alisema.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kusisitiza suala la ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali. Kuhusu mapato, Waziri Mkuu alisema katika mwaka wa fedha wa unaoisha sasa, hali ya ukusanyaji mapato haikuwa nzuri.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu alisema amewaandikia barua Wakuu wa Mikoa akiwataka waweke utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu juu ya makusanyo ya kila Halmashauri zilizo kwenye mikoa yao.
"Katika taarifa hizi itabidi kila Halmashauri ieleze ilipanga kukusanya kiasi gani, je imefikia lengo na kama sivyo ni kwa nini. Nia yetu ni kutrack down makusanyo na kuona yamekwama wapi na yamekwamishwa na nini," alisema.
Kuhusu udhibiti wa matumizi, Waziri Mkuu aliwataka Mameya na Wenyeviti hao kuendelea kuwabana wahusika ili kudhibiti matumizi yasiyofaa. "Lazima muendelee kuwabana na kuwasimamia wakurugenzi na wataalaam wa kwenye Halmashauri zenu. Fanyeni kazi kwa ufanisi, msiwachekee wale wanaoharibu," aliongeza.
"Ili muweze kuwabana vizuri, ni lazima mdai kupatiwa taarifa za fedha kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani (Internal Auditor)... kuna baadhi ya watendaji wanadai kuwa hizi taarifa ni siri wakati siyo siri," alisema.
Aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kwamba taarifa hizo ni muhimu kwao kuzipata na zitawasaidia kuonyesha mapungufu yoyote kama yapo.
Aliwataka kila mmoja wao kwa nafasi zao za Meya na Mwenyekiti wahakikishe wanalenga kupandisha pato la wananchi wanaowaongoza.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JUNI 30, 2014

HAPPY BIRTHDAY MWANDISHI MKUU WA MBEYA YETU BLOG
Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Joseph Mwaisango
******
TONE MULTIMEDIA GROUP Ambao ni wamiliki wa Mtandao huu wa Mbeya yetu Blog , Tunapenda Kuungana na wadau wetu wote Kumpongeza Bwana Joseph Mwaisango ambaye
ndiye Mwandishi Mkuu wa Blog hii ya Mbeya yetu na Mmoja wa wakurugenzi
wa Tone Multimedia Company Limited (TMCL) ambao pia ni wamiliki wa Blogs za Mikoa Tanzania, Tone Radio-Tz , This Day Magazine, Stay In Tanzania(Tanzania Tours) , Tone Tube Tz , Matukio na Wanavyuo na Watanzania waishio nje ya Nchi kwa kutimiza miaka yake kadhaa siku ya Leo.
Tunapenda
kumpa Hongera sana kwa kazi nzito ambazo anazifanya ili kuwaletea wadau
habari zilizo sahihi na za uhakika zaidi kutoka pande zote za Mkoa wa
Mbeya, Pia tunamuombea kwa Mungu ampe siku nyingi zaidi , Afya Njema na
aendelee kuchapa kazi zaidi na zaidi bila kusahau kuongeza Ubunifu
zaidi.
Pia
katika Hili tunapenda kuwashukuru wadau Mbali mbali wa Habari wakiwemo
Bloggers wote wa Tanzania, Magazeti, Radio na TV kwa kuendelea kuonesha
ushirikiano mkubwa ili kazi ziendelee kwa ufanisi mkubwa
Mwisho
tunapenda kumshukuru kila mmoja wetu ambaye ni mdau mkubwa wa Blog ya
Mbeya yetu, wote tupo pamoja katika kusherekea siku hii ya leo.
Asanteni
Na: Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ameonya kuwa vitendo vya hujuma
dhidi ya raia na wageni, vinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa
Zanzibar.
Amesema Zanzibar
ambayo imekuwa ikitegemea zaidi sekta ya Utalii kuendeleza uchumi wake na
kukuza pato la taifa, imekuwa ikiguswa na matukio hayo ya hujuma, na kwamba
yanaathiri uchumi, ustawi wa jamii na sifa ya ukarimu kwa Zanzibar.
Mhe. Maalim Seif
ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha ITV,
Mikocheni Dar es Salaam.
Amesema katika
kukabiliana na vitendo hivyo, serikali inakusudia kutekeleza mpango wake wa
kuweka kamera za CCTV katika maeneo muhimu ya utalii likiwemo eneo la Mji
Mkongwe, ili kuweza kuwabaini kwa urahisi wahusika wanafanya vitendo hivyo.
Kuhusu zao la karafuu
kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibar, Maalim Seif amesema serikali imefanikiwa
kudhibiti magendo ya karafuu baada ya kuongeza bei ya zao hilo na kuwashinda
wanunuzi wengine wa Afrika Mashariki ambako karafuu hizo zilikua zikipelekwa.
Aidha amesema katika
kuhakikisha kuwa ubora wa karafuu za Zanzibar unalindwa na kudhibiti wauzaji
wengine, Serikali kupitia Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, itaweka nembo
maalum “brand”, kuweza kuzitofautisha karafuu za Zanzibar na maeneo mengine.
Akizungumzia dawa za
kulevya, Maalim Seif ambaye ofisi yake ndiyo inayohusika na udhibiti wa dawa
hizo, amesema bado kuna kazi kubwa ya kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa
hizo kutokana na jiografia ya visiwa vya Zanzibar.
Amefahamisha kuwa
vita hiyo pia ni ngumu kutokana na uwezo mkubwa wa wafanyabiashara wa dawa hizo
ambao wanaweza kuwarubuni watendaji kwa pesa nyingi na kuacha kutekeleza wajibu
wao.
Amesema katika kupiga
vita dawa hizo, ni lazima kuwepo na mashirikiano pamoja na uadilifu miongoni
mwa watendaji, hasa wale wanaofanya kazi katika viwanja vya ndege, bandarini na
vyombo vya ulinzi.
Maalim Seif ambaye
pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, amesema Serikali ya Umoja wa
Kitaifa GNU itaendelea kuwepo hata baada ya uchuguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa
vile suala hilo ni la kikatiba na limewekewa misingi maalum.
Kuhusu mchakato wa
katiba mpya, Maalim Seif amesema bado serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa
katiba mpya inapatikana, ili kuendeza ustawi wa Taifa na kukidhi mahitaji ya
wananchi.
Amesema tayari
serikali imeshatumia fedha nyingi za wananchi, na kwamba kushindwa kukamilisha
mchakato huo kwa wakati, itakuwa ni hasara kwa serikali na taifa kwa ujumla.
Hivyo
amesema hakuna budi kwa serikali kutafuta njia mbadala za mazungumzo, kuhakikisha
kuwa mchakato huo unaendelea na unafanikiwa kwa maslahi ya Taifa.
HABARI HII HAINA
PICHA. AHSANTENI WADAU.
Sunday, June 29, 2014
BRAZIL `WACHIZIKA` NA USHINDI WA PENATI DHIDI YA CHILE, SASA NGOMA ROBO FAINALI!
wakishangilia ushindi wao wa
penati 3-2 dhidi ya Chile na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.
WENYEJI Brazil wamekuwa wa kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe
la dunia baada ya jana usiku kuifunga Chile kwa mikwaju 3-2 ya penati
kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida na dakika 30 za
nyongeza.
Kutokana na matokeo hayo, baadhi ya wachambuzi wa soka wameanza kuwa na
wasiwasi na mwendo wa Brazil na kushindwa kutambua watafika hatua gani.
Lakini sapoti kubwa wanayopata kutoka kwa mashabiki wao inaweza kuwa
motisha kubwa kwao na wakajikaza hatua inayofuata.
Jibu...
|
|||
|
|||
|
|||
|
KANISA LA YESU KRISTO LA WATAKATIFU WA SIKU YA MWISH
Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi akiwapatia maelezo mbalimbali kwa watu waliotembelea kanisa hilo wakati wa siku ya wazi kwa ajili ya watu mbalimbali kuangalia shughuli zinazofanywa na kanisa hilo |
Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali
Mwakilishi wa Darasa la Mkono msaidizi wa akina mama Happy Ayubu akitoa maelezo kwa watu waliotembelea kanisa hilo
Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali
Mhumini waKanisa la Yesu Kristo la
Watakatifu wa siku za mwisho Framers Ngosha akijibu maswali ya watu
waliojitokeza katika siku hiyoKiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi 'kulia' akionesha vitabu vinavyotumika kwa ajili ya mafunzo kushoto ni Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi
Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi akitoa maelezo
Baadhi ya watu mbalimbali waliotembelea katika kanisa hilo lililopo Mbezi Beach
Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa
la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba
wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali
iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la
Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi
kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa
lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
watu waliotembelea wakipata mahelezo mbalimbali
Baadhi ya watu waliotembelea katisa hilo
Saturday, June 28, 2014
MATUKIO YA LEO
mbunge wa jimbo la kawe kupitia chadema Halima Mdee akichangia sheria ya sheria ya mswada wa fedha leo mjini dodoma katika kikao cha bunge ambacho kimaharishwa kikao hicho cha bunge |
bado maandalizi ya ya sabasaba picha inaonyesha baadhi ya watu wakiawa na mkokoteni wakipeleka bidhaa kwenye mabanda leo |
baadhi ya wakazi waliofika kwenye maonyesho ya sabasaba yaliyoanza leo kuwahi kununua bidhaa |
Baadhi wa wajumbe waliochaguliwa kuingia Baraza Kuu la Uongozi (CUF) Taifa baada ya kutangazwa rasmi. |
COUTINHO AWASILI
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC Andrey Marcel Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi>
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari walijitokeza kumlaki.
Akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege Coutinho amesema anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi ambayo watu wake wanapenda mpira na kikubwa amekuja kuisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali mbali itayakayowakabili.
Kuhusu changamoto za ugeni katika Bara la Afrika, Coutinho alisema soka kwake ni kazi, ana uzoefu baada ya kucheza pia Barani Asia hivyo hana wasiwasi, na kwa kuwa na walimu aliwazoea anaamini kwa pamoja atafanya vizuri.
Msafara wa kutoka Uwanja wa ndege ulielekea makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani ambapo Coutinho aliwasilimia wapenzi, washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha aliongea na katibu mkuu Bw Beno Njovu kabla ya kwenda kupumzika.
Friday, June 27, 2014
BREEKING NEWZZZZZZ JAMBAZI LAKAMATWA KISIWANI PEMBA ALIUA POLISI NA MGAMBO MKURANGA
JESHI LA POLISI KISIWANI PEMBA LIMEFANIKIWA NA LIMEMKAMATA JAMBAZI MOJA ANAYETUHUMIWA KUVAMIA KITUO CHA POLISI WILAYANI MKURANGA MKOANI PWANI NA WENZAKE NA KUMUUA ASKARI POLISI NA MGAMBO MMOJA NA HATMAYE KUPORA SILAHA NA KUTOKOMEA NAZO JESHI HILO LA POLISI KISIWANI LIMEFANYA KAZI YA ZIADA NA KUMNASA JAMBAZI HILO HUKU JESI LA POLISI WAKIJITAHIDI KUWASA WENGINE RADIO 1 STEREO
MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO ULIPOTEKETEZA SOKO LA KEKO USIKU WA KUAMKIA LEO
Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog
Thursday, June 26, 2014
KOCHA MPYA WA YANGA MAXIMO ATUA DAR LEO MUDA WA SAANA NANE MCHANA
AKISALIMIANA NA WANACHAMA NA WAPENZI WA KLABU HIYO |
AKISALIMIANA NA WANACHAMA NA WAPENZI WA KLABU HIYO |
AKISALIMIANA NA WANACHAMA NA WAPENZI WA KLABU HIYO |
AKIPOKEWA KATIKA KLABU YA YANGA |
AKIONGEA NA WANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA UWANJA WA MWALIM NYERERE LEO |
MAXIMO AKITEREMKA KATIKA KLABU YA YANGA |
MAXIMO AKITEREMKA KATIKA KLABU YA YANGA |
MAXIMO AKIONGEA NA WANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA LEO KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWALIM NYERERE LEO |
MAXIMO AKIONGEA NA WANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA LEO KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWALIM NYERERE LEO |
MAXIMO AKISALIMIANA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUWASILI |
KOCHA MAXIMO AKITOKA NJE KATIKA UWANJA WA NDEGE LEO MCHAANA BAADA YA KUWASILI |
WAPENZI MASHABIKI WA YANGA WALIOFIKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA MALIMU NYERERE KUMPOKEA KOCHA WAO MAXIMO LEO ALIPOFIKA MUDA SAANA NANE MCHANA |
MASHABIKI WA SIMBA WAKISHOBOKEA HUKU WAKITOA MANENO YA DHARAU WAKIWA NJE YA KLABU YAO WAKATI MSAFARA WA KOCHA MAXIMO UKIPITA KATIKA BARABARA YA MSIMBAZI WAKIELEKEA KATIKA KLABU YA YANGA JANGWANI LEO |
KOCHA WA YANGA MAXIMO AKIWASALIMIA WAPENZI NA MASHABIKI WA YANGA MARA BAADA YA KUTEREMKA KWENY KLABU HIYO LEO AKITOKEA BRAZILI |
MAXIMO AKIWASILI KATIKA KLABU YA YANGA JANGWANI AKIWA KATIKA GARILEO |
WAANDISHI WA HABARI NA MASHABIKI WA YANGA WAKIMUHOJI KOCHA MAXIMO MARA BAADA YA KUWASILI LEO KATIKA UWANJA WA NDEGE |
MASHABIKI WA YANGA WAKIWA WAMEJIPANGA KATIKA UWANJA WA NDEGE WANAMSUBIRI KOCHA MPYA MAXIMO AKITOKA WAMPE MKONO LEO |
Subscribe to:
Posts (Atom)