Home » Archives for August 2014
Sunday, August 31, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 31 Ogasti, 2014
Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani.
Taarifa Na.
201408-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 6:00 Mchana
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
01 Septemba, 2014
Mpaka:
Tarehe
02 Septemba, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani.
Kiwango cha uhakika:
Juu: (70%)
Maeneo yatakayoathirika
Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkali wa Kusi, mashariki mwa Pwani ya Tanzania.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

MVU: CCM ITAUPUKUTISHA UPINZANI TEMEKE UCHAGUZI WA MITAA, SIYO KWA NGUVU ILA KWA MATUNDA YA UTEKELEZAJI ILANI
Press ? for keyboard shortcuts
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akihutubia mkutano wa hadhara uliofabyika kwenye Uwanja wa shule ya Sokoine, Temeke jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 30, 2014.
Mtemvu akishangiliwa wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimpa kadi ya Uanachama wa UWT Maridha Rajabu wakati wa mkutano huo, wanachama wapya 45 wa jumuia hiyo walipewa kadi
Mbunge wa temeke, Mtemvu akimtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Mbunge wa temeke, Mtemvu akimpongeza baada ya kumtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Umati wa wananchi ukiwa umefurika wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Azimio, Tatu Hassan akifungua mkutano huo, kwenye Uwanja wa Sokoine Temeke kabla ya kuhutubiwa na Mtemvu
Diwani wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo wakati wa mkutano huo
Ofisa Kutoka Makao Makuu ya CCM, Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Gifti Isaya akipata picha kupitia simu yake kwenye mkutano huo
Waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo. Wapili walioketi kulia ni Ofisa katika Idara ya Mambo ya Nje Makao Makuu ya CCM, Gift Isaya akifuatilia kwa makini pamoja na wenzake
Msanii Yusuf Peter wa Kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha vimbwanga vyake mbele ya mke wa Mbunge wa Temeke Mama Mtemvu (kulia)
Msanii Ahmadi Juma wa kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha uhodari wa 'kula' moto wakati kikundi hicho kikitoa burudani wakati wa mkutano huo
Mtemvu akiwatuza wasanii waliotia fora uwanjani wakati wa mkutano huo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
Wednesday, August 27, 2014
JUKWA LA KATIBA
Jengo la Makao Makuu ya Ofisi za Jukwaa la Katiba.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Hebron Mwakagenda.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa tathimini hiyo. Kulia ni Mratibu wa Jukata, Diana Kidara na Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda (kulia), akionesha Katiba ya Tanzania wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Rodirick Maro na
Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata),
Hebron Mwakagenda (kulia), akisisitiza jambo wakati
akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC), Rodirick Maro na
Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
Mwakilishi kutoka Taasisi ya NKM, Hezron Kaaya (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com. simu namba 0712-727062)
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata),
Hebron Mwakagenda (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wenzake. Kulia ni Mwakilishi kutoka UVIATA,
Martha Mwanyeza.
Mratibu wa Jukata Diana Kidara (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wenzake. Kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Shinyawata, Maria Chale.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata), limemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Samuel Sitta kufuata sheria na kaanuni za bunge hilo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alisema kuwa kwa sasa Sitta hana mamlaka ya kukusanya maoni kwani ni kinyume na sheria ya tume ya mabadiliko katiba.
"Tumeshuhudia bunge maalumu la katiba likiongozwa na mheshimiwa Sitta likiendelea kupokea maoni ya makundi mbalimbali wakiwemo wafugaji, waandishi wa habari na wasanii ambapo ni kinyume na sheria," alisema.
Mwakagenda alifafanua kuwa hatua hiyo imekwenda kinyume cha sheria namba 9 (1) ambacho kinaeleza kazi za tume ya mabadiliko ya katiba ambayo ilikuwa na kazi ya kukusanya, kuchambua, kuandika taarifa na kuwasilisha kwenye bunge ambapo kazi yake ni kuipitisha kama ilivyo kwenye kifungu cha sheria namba 25.
Katika suala la uondoaji wa vifungu kwenye rasimu hiyo alisema rasimu imezingatia kero na malalamiko ya wananchi hivyo kuyaondoa ukilinganisha na mantiki inayoendelea bungeni ni sawa na kurekebisha katiba ya mwaka 1977 na kubaki na malalamiko kwa wananchi kuwa viongozi hawawajibiki.
Pia aliyataka makundi yanayopingana kwenda kwenyekikao kinachotarajiwa kufanyika Ikulu wiki hii kwa moyo mkunjufu na kwa kuzingatia maslahi ya taifa na si vyama vyao.
Hata hivyo alisema kuwa pamoja na juhudi za kuendeleza mchakato wa katiba mpya lakini mchakato huo hautokamilika na kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alifafanua kuwa hali hiyo imesababishwa na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kiserikali zikiwemo za uandikishaji mpya wa vitambulisho vya kupigakura katika mfumo mpya wa BVR.
Pia alisema kuwa kupanda kwa joto la uchaguzi kwa sasa pia inaweza kusababisha katiba kutopatikana kwani takribani wanasiasa wote wamegeukia kwenye uchaguzi na si kupatikana kwa katiba.
"Sisi kama Jukata tunashauri mchakato huu kuhairishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu na kuanza tena januari 2016 ili kuokoa gharama za uchaguzi kwa kuunganisha na kufanyika chaguzi zote kwa mara moja," alisema Mwakagenda.
Reply, Reply All or Forward | More

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATUA NCHINI, KESHO KUENDESHA MHADHARA HOTELI YA PROTEA COURT YARD SEAVIEW JIJINI DAR ES SALAAM
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akimtambulisha kwa madaktari (hawapo pichani), Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani ya matiti, Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole India, Dar es Salaam jana. Daktari huyo kesho jioni anatarajia kufanya mhadhara na madaktari wa Kitanzania na wadau wa sekta ya afya kujadili ugonjwa huo katika Hoteli ya Protea Court Yard. Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa Kimataifa.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa na daktari huyo (katikati), Kushototo ni Mama Benedicta Rugemalira. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Profesa Anthony Pais (katikati), akizungumza na madaktari wa Tanzania. Kushoto ni Dk.Maleare na Dk. Fredy
Profesa Anthony Pais (kulia), akizungumza na madaktari wa Tanzania.
Wadau wa sekta ya Afya wakiagana na daktari huyo nyumbani kwa Mshauri wa Kujitegemea wa Kimataifa, James Rugemalira Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Dotto Mwaibale
DAKTARI Bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti ,
Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole nchini India kesho Agosti 28, 2014 anatarajia kutoa muhadhara kuhusu ugonjwa
huo.
Akizungumza na Mtandao wa www.habari za jamii.com. Dar es Salaam leo
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira alisema ujio wa daktari
huyo hapa nchini ni fursa kwa watanzania kutokana na changamoto kubwa iliyopo
kuhusu ugonjwa huo.
"Daktari huyu amebobea katika ugonjwa wa
saratani ya matiti na amefanya operesheni nyingi za ugonjwa huo ni wakati mzuri
kwetu kwenda kumsikiliza kesho jioni Hoteli ya Protea Court Yard" alisema Rugemalira.
Alisema kesho daktari huyo atatoa mhadhara kwa
madaktari wa kitanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo na jinsi
ya kukabiliana nao.
Rugemalira alisema daktari huyo atakuwepo nchini
kwa siku kadhaa na leo alitembea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya
Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa
mshauri huyo wa kimataifa ili kuona namna ya kusaidia tatizo hilo.
Tuesday, August 26, 2014
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akijaribu kuwasha moja ya magari hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid(kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Kitabibu wa Ilala, Dk.Mbarouk Seif.
Dotto Mwaibale
SERIKALI imepokea msaada wa magari manne na pikipiki 20 zenye thamani ya sh. .261,105,615 kutoka Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA) kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.
Akipokea msaada huo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema Tanzania imefikia lengo la kimataifa la kutokomeza ukoma kwa kuwa chini ya mgonjwa mmoja katika watu 10,000 hivyo kufanya ukoma kutokuwa tatizo kubwa la afya nchini.
Alisema pamoja na kupokea msaada huo bado kumekuwa na changamoto ikiwemo za ukosefu wa magari na pikipiki kwa mikoa na wilaya mpya ambapo Serikali kupitia mpango huo unafanya jitihada za kupata vyombo vya usafiri katika mikoa hiyo.
Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitapelekwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Halmashauri za Ilala na Kinondoni ambapo aliomba vitumika vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
"Napenda kuuwaasa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya vyombo hivi vya usafiri kwa kuhakikisha wale wote watakaokabidhiwa wanavilinda kwa kuvitumia vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa na kwa kufuata taratibu za serikali na si vinginevyo," alionya.
Dk. Rashid alitoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuangalia namna ya kuchangia gharama za matengenezo ya vyombo hivyo ili kuziba pengo la kupungua kwa misaada inayotolewa na wahisani.
More

Saturday, August 23, 2014
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya masai safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa
watakayozindua siku ya
August
30 katika ukumbi wa raunch time ya jijini akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki
alizitaja nyimbo zilizomo katika albam
hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba
albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni
mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio
zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu
aliongeza kwa kutaja wasanii wengine
watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii
mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi uho
bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo
Friday, August 22, 2014
Onyesha Uzalendo Wako - Real Madrid vs Taifa Stars
About Onyesha Uzalendo Wako - Real Madrid vs Taifa Stars:
ONYESHA UZALENDO WAKOKuona sio sawa na kuhadithiwa, fikiria unawaona magwiji wa Real Madrid kama Luis Figo mita chache kutoka ulipokaa pale uwanja wa Taifa Jumamosi ya tarehe 23.8.2014.Unakosaje burudani hii? ?#?GameoftheYear? ?#?RealMadridvsTaifaStars? ?#?VodacomTaifaStars? Kuwa nasi katika ukurasa huu tukitoa wasifu wa magwiji hawa.
Location/Directions:
Uwanja wa Taifa / The National StadiumRAIS KIKWETE AWEKA AFUNGUA KITUO CHA AFYA KIBAONI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea akikagua wodi mpya ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kituo cha Afya cha Kibaoni
Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
PICHA NA IKULU
|
Subscribe to:
Posts (Atom)