Home » Archives for September 2014
Tuesday, September 30, 2014
26 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA BENIN
Wachezaji
26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili
mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha
Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini
Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki
ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga),
Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam),
Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda
(African Lyon).
Viungo
ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri
Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla
(Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji
ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa
(Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
MKUTANO WA SIKU MBILI JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI, UHAKIKA WA CHAKULA NA HAKI ZA ARDHI ULIOANDALIWA NA OXFAM PAMOJA NA FORUM CC WAANZA LEO
Jenerali Ulimwenguambaye ndiye mwezeshaji akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.
Meza ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.
Kushoto ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi Muwekezaji alivyo wanyang'anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate rudishiwa Ardhi yao.
Kushoto ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
Mlalamikaji Mwengine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi jinsi ya eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa warudishiwe
Mmoja wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya njaa.
Mchangiaji kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
Mmoja wa wachangiaji akizungumza Jambo
Mh. Jaji Richard Mzilay Akitoa Maelezo ya kina juu ya Walalamikaji kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu ambapo walikuwa wanataka Eneo lao lirudishwe, Ametoa maelekezo ya yale ambayo wanatakiwa wayafuate.
Washiriki wa Mkutano huo
Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
Burudani Elimisha ikiendelea
Wadau wameguswa na kujumuika kucheza
Picha ya pamoja
Monday, September 29, 2014
BREKING NEWZZZ WATU ZAIDI YA 200 WANUSURIKA KUFA
ZAIDI YA WATU WAPATAO 200 WAMENUSURIKA KUFA BAADA YA KUNYWA KINYWAJI AINA YA TOGWA KINACHODHANIWA KUWA NA SUMU KATIKA KIJIJI CHA CLITAPWASI MKOANI RUVUMA LEO HABARI ZAIDI TUTAWALETEA SOMA BLOG YA MZUKA
TAASISI YA VYOMBO VYA HABARI KUSINI MWA AFRIKA(MISA-TAN) YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA KUTOA MATOKEO YA UTAFITI WA UPATIKANAJI WA TAARIFA KWENYE OFISI ZA UMMA NCHINI TANZANIA
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto)
akiwakaribisha wageni waalikwa na waandishi wa habari waliofika kweye
mkutano wao uliofanyika Jana kwenye ofisi za MISA Tanzania zilizopo
jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew.
Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Jana imekutana na waandishi wa habari na wadau tofauti katika kuadhimisha Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.09.2014 katika ofisi zao zilizopo kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.
Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Jana imekutana na waandishi wa habari na wadau tofauti katika kuadhimisha Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.09.2014 katika ofisi zao zilizopo kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia)
akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kwenye
siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28
kwa kila mwaka.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wagene waalikwa (hawapo pichani) kwenye
siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28
kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege (kushoto) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la
ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa
nchini.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege akiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kitabu
cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Kofuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege akionesha tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014 iliyokwenda kwenye Idara ya Mahakama.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu kwa mwaka 2014 kwa kutoa taarifa bila kificho kwa mwaka 2014
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon
Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu Kaimu Mkurugenzi
wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda
Komba(kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata
taarifa jana jijini Dar es Salaam
Kaimu
Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi.
Aldegunda Komba akionesha tuzo hiyo kwa waandishi wa habari pamoja na
wageni waalikwa waliofika kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi.
Aldegunda Komba akizungumza na vyombo vya habari baada ya taasisi
yaokutwaa tuzo ya Ufungu wa Dhahabu.
Afisa utafiti na maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kwenye siku ya kimataifa ya
haki ya kupata taarifa ambayo uadhimishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
Baadhi
ya wageni waalikwa pamoja na waandhishi wa habari wakifuatilia shughuli
zima iliyokuwa inaendelea kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi
ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo jijini Dar es Salaam.
Siku Ya Kimataifa Ya Haki Ya Kupata Taarifa
msama promotion atoa msaada
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) Alex Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
"Mimi na familia yangu tutatoa milioni 1".
Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Usharika huo ulitoa ahadi ya sh. laki 7.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akipokea mchango wa Usharikia wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Christosiler Kalata .
Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
Watu mbalimbali waliahidi kutoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Edson Mwasabwite alichangia kiasi cha sh. laki moja.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MJUMBE wa Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika
Segerea.
Msama ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha
ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam,
huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.
Akizungumzia ushuhuda huo,
Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma,
kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.
"Unajua mimi katika
maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye
mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva
taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda
muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.
Msama ambaye ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali
aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa
hai.
Harambee hiyo iliyoenda
sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama
Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.
Mbali ya kiasi hicho
alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na
kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.
Subscribe to:
Posts (Atom)