Friday, October 31, 2014

KITUO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA WASHIRIKI ALHAMISI YA BURUDANI

0 comments

 Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akitoa mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development) iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke.

Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao
 Mkutubi - Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,  Harriet Macha akisisitiza jambo kwenye mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevubaada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development)
 Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe,   Ismael Mnikite akizungumza jambo kuhusu mada husika na kuangalia ni njia  gani zinaweza kuwapelekea vijana kushiriki kwenye shughuli nzima za maendeleo
Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe,   Ismael Mnikite akigawa vipeperushi vya Umoja wa mataifa pamoja na fomu kwa vijana hao wa Temeke.
Mada ikiendelea
Katibu wa Mtandao wa Vijana Temeke,  Yusuph Kutengwa akichangia mada
 Omari A. Mketo akichangia
 Ishengoma ambaye ni mlemavu wa macho akieleza faida alizozipata baada ya kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kutoa mafunzo hayo kwa mtandao wa vijana wa Temeke.

Baadhi ya vijana wa mtandao wa vijana wa Temeke wakisoma kwa umakini malengo ya milenia wakati kituo cha habari cha umoja wa mataifa walipokuwa wanatoa mada kwa vijana hao
Picha ya pamoja
Endelea Kusoma >>

MAKINDA ATTENDS THE OFFICIAL OPENING OF THE 36 SADC PF ASSEMBLY IN VICTOR

0 comments
The Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda adoring the speech from the Guest of honor during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab and the SADC PF treasure Hon.  Seleman  Said Jaffo

 Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda keenly listening attentively to the Opening speeches during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab

 Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda keenly listening attentively to the Opening speeches during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab

Members of the Tanzania Delegation to the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum listening attentively the official opening of the Assembly in Victoria Falls Zimbabwe. From Right is Hon. Habib Mohamed Mnyaa, Hon. Anna Abdalah and the Director of Civic Education, Information and International relations from the Parliament of Tanzania Mr. Jossey Mwakasyuka

The SG of the SADC PF Dr. Essau Chiviya delivering his introductory statement during the Official Opening

The Guest of Honor who is the Minister for Justice, Legal and Parliamentary Affairs of Zimbabwe Hon. Emmerson Mnangagwa delivering his Opening Speech

A welcoming speech from the Speaker of the Parliament of Zimbabwe Hon. Jacob Mudenda     Photos by Owen Mwandumbya



Endelea Kusoma >>

ALIEKUWA MTANGAZAJI NA MWANDISHI WA HABARI RADIO TANZANIA SASA TBC BEN KIKO AFARIKI DUNIA

0 comments





Katibu wa Rais maswala ya Habari, Issa Michuzi kulia akiwa na mtangazaji wa siku nyingi, Beni Kiko wakifurahia jambo wakati wa uhai wake katika tuzo za mwandishi bora 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenela Mukangara kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko.
Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea Hospitali ya Jeshi ya Milambo Mkoani Tabora.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mwanahabari na Mtangazaji huyu Mahiri ambaye ametoa mchango mkubwa wa kihabari kwa Taifa letu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba wa Ben Hamis Kikoromo.
“Namkumbuka Marehemu Ben Kiko, enzi za uhai wake, kama Mtangazaji aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa wasikilizaji wake kutokana na namna yake ya kipekee ya kuripoti matukio hususan katika kipindi kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati huo cha MAJIRA kilichokuwa kikirushwa hewani na  Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)”.
 Wakati wa vita dhidi ya Nduli Idi Amin wa Uganda mwaka 1978, Ben Hamis Kikoromo alifanya kazi kubwa kwa Taifa kwani aliweza kuripoti matukio mbalimbali kutoka katika uwanja wenyewe wa vita, na hivyo kuliwezesha Taifa na wananchi kwa ujumla kuhabarika vilivyo na matukio yaliyokuwa yakiendelea.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, pokea salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa Waandishi na Watangazaji Mahiri katika Tasnia ya Habari hapa nchini. 
Vilevile kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo kwa kupoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti wa Familia.  Nawaomba Wanafamilia wote, ndugu na Jamaa wa Marehemu wawe wavumilivu na wenye subira wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao huku wakitambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.
  Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika muda wote wa maombolezo, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo, Amina.
Aidha Rais Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kwa Wanahabari kote nchini ambao kwa hakika msiba wa Ben Kiko utakuwa umewagusa kwa karibu. 
Hata hivyo amesema kuondoka kwa Ben Kiko kusiwe chanzo cha wao kukata tamaa, bali kifo chake hakina budi kuwa chachu katika kujituma zaidi, na wawe tayari kuiga yote mazuri aliyoyafanya Marehemu enzi za uhai wake hapa duniani hususan katika Taaluma ya Uandishi wa Habari.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Oktoba, 2014.


Endelea Kusoma >>
0 comments

Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu

      


D92A1998Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro). D92A1988Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja  na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro)
Endelea Kusoma >>

Thursday, October 30, 2014

AJALI MBAYA YA ARUSHA

0 comments


Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde. 









Endelea Kusoma >>

Wednesday, October 29, 2014

BREKING NEWZZZZZZZZ WATU 9 WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO LE JIONI

0 comments
Watu 9 wamefariki dunia na wengine 2 wamejeruhiwa baada ya basi dogo la abiria Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta katika eneo la makumira wilayani Arumeru kwa mujibu wa kamanda wa polisi Arusha libaratus Sabas ametibitisha na kusema imetokea mida ya saa kumi leo lori hilo namba ya usajili T582 ACR likitokea mkoani kilimanjari na kwenda Arusha majeruhi wamepelekwa katika hospitali iliyokaribu ya Tengeru  na waliofariki miili yao imehifadhiwa katika hospitali  ya Mount Meru  RADIO ONE STEREIO  TUTAWALETEA HABARI ZAIDI KATIKA MZUKA WA FUNGO


Endelea Kusoma >>
0 comments
BONDIA FADHILI MAJIHA AONESHA MAAJABU KWA KUPIGWA KWA POINT THAILAND MCHEZO WA RAUNDI 12





Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point

 Na Mwandishi Wetu


akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi

bondia huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe

nimerudi nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali yangu 
nae  Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne
Endelea Kusoma >>

RAIS WA ZAMBIA AFARIKI DUNIA

0 comments
Rais wa Zambia Michael Sata amefariki dunia nchini uingereza alikokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa ambao mpaka kifo chake haijawekwa wazi kuwa alikuwa anaumwa nini.

Rais Sata ambae alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mfalme Edward VII amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 77.

Taarifa zinasema rais huyo wa Zambia aliaga dunia baada ya mapigo ya moyo kupanda ghafla.

Hakuna taarifa ya mara moja juu ya mtu atayemrithi Rais Sata,suala hilo litaamuliwa na baraza la mawaziri la nchi hiyo linalotarajia kukutana leo Jumatano asubuhi.

akitangaza kifo cha rais huyo,katibu wa baraza la mawaziri Roland Msiska kwenye televisheni ya taifa ya nchi hiyo,alisema kwa masikitiko na mshtuko mkubwa,natangaza kifo cha rais wetu mpendwa Michael Sata.

Aliongeza kwa kusema kuwa mke wake na mtoto wake wa kiume walikuwa pembeni yake wakati rais huyo anakata roho.

Akawataka wazambia wote kuwa watulivu,wamoja kwa kipindi hiki kigumu cha msiba uliolikumba taifa hilo.

kifo cha Rais Sata kimekuja siku chache baada ya Zambia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waingereza.

Rais Sata anakuwa Rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani mwingine alikuwa ni Levy Mwanawasa alifariki dunia mwaka 2008.

Balozi wa Zambia hapa nchini Jdith Kangoma-Kapijimpanga  kulia akiongea na wandishi wa habari hawapo pichani kuhusu kifo cha Rais huyo kilichotea leo nchini Uingereza

Endelea Kusoma >>

Tuesday, October 28, 2014

CHID BENZ APANDISHWA KIZIMBANI JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA,AKOSA DHAMANA, KESI YAKE KUTAJWA TENA NOVEMBA 11

0 comments
picha akisindikizwa na askari polisi wa mahakama ya kisutu leo 

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29),maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz amefikishwa mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.
Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka yake.Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo itakapotajwa.
Chanzo;michuzi blog
 

Endelea Kusoma >>

Monday, October 27, 2014

BONDIA SAIDI MBELWA APIGA GEORGE DIMOSO KWA POINT

0 comments
S

BONDIA SAIDI MBELWA APIGA GEORGE DIMOSO KWA POINT

Bondia Georger Dimoso kushoto akipambana na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamoso iliyopita Mbelwa alishinda kwa point mpambano huo wa raundi nane Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba na Geore Dimoso wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi jana Mbelwa alishinda kwa point Picha na SUPER D BLOG


 Mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakifatilia kwa makini mchezo huo
Bondia Said Mbelwa akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wa mpambano huo

Bondia Hamza Mchanjo kushoto akipambana na Juma Fundi wakati
wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Fundi alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BLOG
Baadhi ya mashabiki kutoka Tanzani Boxing Fans Group Watssup wakijadili jambo na bondia Thomasi Mashali wa pili kushoto anae ongea nae ni Rajabu Mkamba mwenye tai
Bondia Aman Bariko 'Manny Chuga' akioneshana umwamba na Ally Bugingo wakati wa mpambano wao Bariki alishinda kwa point picha na SUPER D BLOG

Bondia Zamoyoni Mbishi kushoto akipambana na Sadiq Nuru wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mbishi alishinda kwa pointi picha na SUPER D BLOG


Bondia Hassan Mandula kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mohamed Jaka Mandula alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na SUPER D BLOG
Endelea Kusoma >>

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA WASANII KWENYE MADHIMISHO YA SIKU YA MSANII

0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam

 


Wasanii wa ngoma kutoka Ukerewe wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo

Msanii wa tasnia ya taarab Isha Mashauzi na kikundi chake nao walikuwepo kwenye maadhimisho ya siku ya msanii Mlimani City.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Josephat Kanuti msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini,   kwenye
maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam

 



Wasanii wa kikundi cha sarakasi nao walionesha umahiri wao kwenye usiku wa maadhimisho hayo.

 

Wasanii wa kikundi cha sarakasi nao walionesha umahiri wao kwenye usiku wa maadhimisho hayo.

 

Msanii Daimond na kikosi chake wakifanya vitu vyao kwenye maadhimisho hayo.
 

Wasanii na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye ukumbi huo. (Picha na OMR)
 

Msanii Daimond na kikosi chake wakifanya vitu vyao kwenye maadhimisho hayo.
 

Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu