Wednesday, December 31, 2014

0 comments

KOCHA MPYA SIMBA ATUA DAR, AKATAA KUIZUNGUMZIA YANGA



Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic ametua jijini Dar es Salaam, tayari kuanza mazungumzo na uongozi wa Simba.

Lakini Kuponovic amekataa katakata kuizungumzia Yanga na kusema akili yake ni Msimbazi.

"Siwezi kuizungumzia Yanga, najua mambo ya upinzani yapo lakini kwa sasa naelekeza nguvu zangu katika mechi ya kwanza.

"Kama nitasaini na Simba, basi nitaangalia nitafanya nini katika mechi ya kwanza," alisema Kopunovic raia wa Serbia mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Endelea Kusoma >>

mtaani

0 comments
hivinndivyo hakli ya daraja lwa mwendo kasi huku wafanyabiashara mama lishe pamoja na watu wengine wakendesha biashara zao kamera ya

mzuka wa fungo alivyoinasa leo
Endelea Kusoma >>
0 comments

TMA YATOA TAARIFA JUU YA MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JANUARI, FEBRUARI, 2015 NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, kuhusu mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Januari na Februari, 2015 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi, Huduma za Utabiri, Dk.Hamza Kabelwa.
Wana habari wakiwa kwenye mkutano huo leo
..........................................................................

Habari/ Picha na Dotto Mwaibale

SIKU moja baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa za vipindi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agness Kijazi Dar es Salaam jana wakati akiwasilisha tathmini ya mvua za vuli kuanzia Ocktoba hadi Disemba mwaka huu na mwelekeo wa mfumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha Januari na Febduari 2015.
Alisema kutokana na mifumo iliyopo ya hali ya hewa inatarajiwa kusababisha vipindi vya ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya Magharib kwenye mikoa ya, Nyanda za juu Kusini-Magharibi na mikoa ya Kusini mwa nchi kuanzia Januari na Febduari 2015.
Hata hivyo alisema kuwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka hususan Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki, Pwani ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa Viktoria na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma mvua zinatarajia kuisha mwishoni mwa Disemba mwaka huu.
Alisema matukio ya mvua katika maeneo ya mvua za nje ya msimu yanatarajiwa katika kipindi cha miezi ya Januari 2015.Hali hiyo inatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Kusini mwa Mkoa wa Pwani na baadhi ya meneo ya Mikoa Arusha , Manyara, Kagera, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Dk. Kijazi alisema katika maeneo mengine yaliyosalia yanatarajia kuwa makavu huku maeneo ya Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini-Magharibi, Kusini mwa nchi na Pwani ya Kusini ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
"Izingatiwe kuwa pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa katika maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani, hali hiyo pia itajitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani," alisema.
Aliongeza kuwa matukio ya vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini.
"Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani," alisema.
Endelea Kusoma >>
0 comments
Endelea Kusoma >>

Tuesday, December 30, 2014

0 comments
THE MBONI SHOW YAANZA KUUNGURUMA JANUARY 2 NDANI YA TBC

Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.
Endelea Kusoma >>

Monday, December 29, 2014

MAALIMU SEIF SHARIFF HAMADI AUNGURUMA UNGUJA

0 comments
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Mhe. Mansour Yussuf Himid baada ya kuamua kujiunga na chama hicho na kumkabidhi rasmi kadi ya CUF katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja



MKOA WA KUSINI UNGUJA.                              
Na: Hassan Hamad (OMKR).
Aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mansour Yussuf Himid, amejiunga rasmi na chama cha wananchi CUF.
Mhe. Mansour ambaye amewahi kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushika nyadhifa mbali mbali ikiwemo ya Waziri wa Kilimo, amechukua uamuzi huo leo kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Baada ya kukabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Mhe. Mansour amesema ameamua kujiunga na CUF baada ya kubaini na kuridhika kuwa chama hicho kimebeba matumaini mapya ya wazanzibari.
Mhe. Mansour ambaye tayari alishateuliwa na chama hicho kuwa mshauri wa mikakati wa Katibu Mkuu wa CUF, amechukua kadi hiyo akiwa miongoni mwa wanachama wapya 108 waliojiunga na CUF kwenye mkutano huo.
Mapema akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza Mhe. Mansour kwa kuamua kujiunga na chama hicho hadharani, na kukiita kitendo hicho kuwa ni cha kijasiri.
Akizungumzia mafanikio ya chama hicho, Maalim Seif amesema kimepata mafanikio makubwa katika mwaka unaomalizika wa 2014, na kutangaza maazimia mapya ya chama hicho kwa mwaka 2015.
Ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kuendelea kukubalika kwa chama hicho katika pembe zote za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Kuhusu maazimio ya Chama hicho kwa mwaka 2015, Maalim Seif amesema kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi mkuu ujao na kuweza kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa.
Hata hivyo amewataka wanachama wasibetweke kutokana na mafanikio yaliyopatikana, bali waongeze nguvu kuhakikisha kuwa malengo ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao yanafikiwa.
Ameongeza kuwa CUF pia kimejipanga kuimarisha uchumi na kujenga Zanzibar mpya itakayokuwa ya matumaini kwa Wazanzibari wote.
Katika hatua nyengine, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika uchaguzi mkuu ujao hatowazuia vijana kutetea haki yao iwapo watadhulumiwa.
“Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nilifanya kazi kubwa ya kuwazuia vijana wasifanye vurugu pale hoteli ya Bwawani. Mwanzo niliwatuma wasaidizi wangu waende kuwaondosha lakini hakuna aliyesikia hadi nilipokwenda mwenyewe, tena waliondoka kwa shingo upande kabisa. Kwa hivyo uchaguzi mkuu ujao sina namna yoyote ya kuwazuia vijana kutetea haki yao”, alifafanua Maalim Seif.
Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kukagua uhai wa chama hicho katika vijiji vya Michamvi, Bwejuu, Jambiani na Paje ambako aliweka mawe ya msingi kwenye matawi ya chama hicho, pamoja na kupandisha bendera kwenye barza ya DAY OUT ya Paje.
………………………………………………………………………………………





Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, baada ya  kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.

.   Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akizungumza na wanachama wenzake , baada ya  kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.

.   Wanachama wa CUF wakionyesha kuunga mkono uamuzi wa Mansour Yussuf Himid kujiunga rasmi na chama hicho kwenye viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja. (Picha na Salmin Said, OMKR).

Endelea Kusoma >>

Sunday, December 28, 2014

YANGA 2 AZAM 2 PAMBANO KATIKA LIGI KUU YA VODACOM

0 comments
Wafungaji wa magoli ya Yanga, Simon Msuva (kushoto) na Amis Tambwe, 
 wakishangilia. 
 
 
 Wachezaji wa Azam, wakishangilia bao lao lililofungwa na Didier Kavumbagu
 
 
 PAMBANO LA LIGI KUU YA VODACOM LIMEMALIZIKA MCHEZO KUMALIZIKA KWA SARE YANGA 2 AZAM 2 MAGOLI YALIFUNGWA NA UPANDE WA YANGA NI AMIS TAMBWE KIPINDI CHA KWANZA NA SIMON MSUVA KIPINDI CHA PILI KWA YANGA NA NA AZAM NI DIDIEKAVUMBAGO KIPINDI CHA KWANZA NA JOHN BOKO KIPINDI CHA PILI
Endelea Kusoma >>
0 comments
KIPINDI CHA PILI  YANGA 2 ZAM 2

*WANAOANZA KUKIMBIZA MTANANGE WA YANGA v/s AZAM TAITAIF


YANGA:- 
Deogratias Munishi, Juma Abdul, Edward Charles, Mbuyu Twite (c), Kelvin Yondani, Salim Telela, Simon Msuva, Haruna 

Niyonzima, Amisi Tambwe, Kpah Sherman na Dan Mrwanda.

BENCHI LA AKIBA:-
Ally Mustafa, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Hassan Dilunga, Hussein Javu, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho.

AZAM FC:- 
Mwadin Ali, Himid Mao, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Didier 

Kavumbagu, Kipre Tchetche na Brian Manjwega.

BENCHI LA AKIBA:- 
Jackson Wandwi, John Bocco, Amri Kiemba, Kelvin Friday, Waziri Salum, David Mwantika na Khamis Mcha.
Endelea Kusoma >>
0 comments


*MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MBANJA NA RASIBURA HUKO LINDI MJINI   

  Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura 
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama Salma alitembelea tawi hilo jana kwa ajili ya kukagua kazi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo.
 Katibu wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisoma maelezo yaliyoko kwenye jiwe la msingi la shina la wakereketwa Zahanati Kempu mara baada ya kuzindua rasmi shina hilo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Endelea Kusoma >>

MSIBA SHEKHE ALI MZEE COMORIAN AMEFARIKI DUNIA MCHANA LEO KUZIKWA KESHO JUMATATU SAA NNE ASBUHI

0 comments
Shekh Ali Mzee Comorian [pichani] amefariki dunia  leo mchana  nyumbani kwake mtaa wa kariakoo jijini Dar es salaam shughuli za maziko zinafanyika  hapo hapo  nyumbani kwake mtaa wa kariakoo Habari Ziwafikie ndugu,jamaa,marafiki, majirani popote pale walipo  Maziko yatafanyika kesho Jumatatu muda wa saa nne Asbuhi  Atasaliwa katika msikiti Makonde na  maziko  katika viunga vya Wangazija mtaa wa Bibi TitiMohamed Jijini Dar EsSalaam  Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti  Imetolewa na Abdulrahamani Mbamba


Endelea Kusoma >>
0 comments
SOMALIA kiongozi mkuu wa kundi la wapiganajani Alshababaab amekamatwa karibu na mji mmoja uliyopo mpakani kati ya kenya na Somalia
Endelea Kusoma >>

Saturday, December 27, 2014

0 comments

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE

      

Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Diamond akiwachombeza mashabiki.
Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.
Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.
Mfalme Mzee Yusuf on da stage.
Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.
Platnumz akizidi kufanya yake stejini.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.
Diamond na Idris wakifanya yao stejini.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.
Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.
Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.
Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.
…Sebene time.
Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.
NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.
Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.

Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)
Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu