*KINANA AUNGURUMA JIMBO LA MTAMBWE ALIKOZALIWA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD WA CUF, AZINDUA MIRADI YA UMEME, MAJI
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiweka kifaa cha umeme kwenye
transfoma wakati wa uzinduzi wa uwekaji nguzo za umeme katika Kijiji cha
Chanjaani, Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba,
wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya
maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Zanzibar
leo. Jimbo hilo ndilo alikozaliwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi
(CUF), ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalimu Seif
Sharrif Hamad.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiweka kifaa cha umeme kwenye
transfoma wakati wa uzinduzi wa uwekaji nguzo za umeme katika Kijiji cha
Chanjaani, Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba,
wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya
maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Zanzibar
leo. Jimbo hilo ndilo alikozaliwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi
(CUF), ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif
Sharrif Hamad.
Komredi
Kinana akihutubia katika mkutano wa halmashauri Kuu ya Wilaya ya Wete,
ambapo alisomewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mkoa wa
Kaskazini Pemba na wilaya hiyo.
Kinana
akipata maelezo kuhusu zao la karafuu alipokwenda kuona ununuzi wa
Karafuu katika Ghala la Serikali la ZSTC, wilayani Wete leo.Kushoto ni
Mkulima wa zao hilo na Issa Hassan ambaye ni Meneja Utawala wa ZSTC.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Jengo la Ofisi za CCM Tawi la Bopwe, mjini Wete. |
Katibu
Mkuu wa CCM, Komredi Kinaa akishiriki kupaka rangi majiko ya Mseredani
(majiko ya mkaa yanayotengenezwa kwa udongo) katika kikundi cha vijana
Jimbo la Gando, wilayani Wete.
Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana ukielekea Jimbo la Mtambwe kwa
kutumia barabara ya kisasa iliyojengwa na Selikali katika Jimbo hilo
alilozaliwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharrif
Hamad. Katika jimbo hilo Kinana alizindua pia mradi wa utandazaji wa
bomba lamji na usimikaji wa nguzo za umeme.
Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM wakifukia mabomba ya maji safi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Jimbo la Mtambwe, wilayani Wete. |
Kinana
akimsikiliza Mwenyekiti wa Maskani ya Chekea iliyopewa jina na Dk,
Jakaya Kikwete katika Jimbo la Mtambwe ambapo vijana wa CUF 35 wamehamia
CCM. Vijana hao walidai wameamua kuhamia CCM baada ya kuchoshwa na
ahadi hewa za viongozi zikiwemo za Maalim Seif Sharrif Hamad. Pia
wameahidi kuwashawishi vijana wengine wa CUF kujiunga na CCM.
Vijana
wa Mtamwe wakishangilia baada ya Mbunge wa CCM Viti Maalumu, kuwaahidi
mbele ya Kinana kuwa atawapatia jezi seti mbili kwa ajili ya mchezo wa
soka.
Kinana
akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud
pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi walipowasili kwenye Chuo cha
Ualimu cha Benjamini Mkapa kuzungumza na Serikali ya wanafunzi wa chuo
hicho.
Mtoto
wa Hayati Abeid Amani Karume, Ali, akihutubia wananchi mjini Wete
ambapo aliwaomba kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa Aprili
30, mwaka huu kwani ina mambo mengi yenye manufaa kwa wazanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa Uoja wa Vijana wa CCM, Shaka, akihutubia katika mkutano huo wa hadhara .
Wafuasi wa CCM wakicheza kwa furaha katika mkutano huo
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo. |
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano huo uliofanyika eneo la Mtemani, Mjini Wete.
0 comments:
Post a Comment