Ali Kiba ahidi makubwa
Sauti za Busara Februari 12
Ali Kiba atamba kufanya
kweli Sauti za Busara mwaka huu
Ali Kiba kupiga shoo ya
'live' Sauti za Busara Feb 12
Na Andrew Chale
Mkali wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali
watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia
kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
Ali Kiba alieleza hayo
leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara
Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa
'Live', ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa
burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Akizungumza mbele ya
wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina
na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
"Hii itakuwa ni
zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba 'live' bila kutumia 'cd' kama
wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga
muziki wa nguvu jukwaani" alisema Ali Kiba.
Na kuongeza kuwa, kwa
sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi maalum kwa
ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani muziki aliusomea na
kujifunza huko nyuma alipokuwa katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo
alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa bendi na 'live'.
Aidha, aliwaomba wapenzi
na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi
kushuhudia tamasha hilo
kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
·
Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa
wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni ishara ya Umoja na Amani, kama
Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inavyohimiza amani.
|
.
0 comments:
Post a Comment