Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Rais Jakaya
Kikwete, akipungia wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam, akitumia gari maalum la kijeshi huku akisindikizwa
na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais aliongoza
watanzania kwenye sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar. Katika sherehe hizo ambazo kauli mbiu yake ni "Tudumishe
mshikamano wetu, pigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa",
zilihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, wananchi lukuki, na viongozi
mbalimbali ambapo zilipambwa kwa gwaride maridhawa la vikosi maalum vya
kijeshi, ikiwemo halaiki. Hali kadhalika ngoma za kitamaduni kutoka bara
na visiwani, zikiwemo kwaya nazo zilinogesha sherehe hizo. Kama kawaida
ndege vita nazo zilitawala anga la uwanja wa Uhuru. |
0 comments:
Post a Comment