2


SI LA KULIKOSA

Friday, May 8, 2015

BBC SWAHILI UINGEREZA CAMERON NA CONSERVATIVES WAONGOZAWaziri mkuu David Cameron anaelekea kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Uingereza hiyo jana.
Chama chake cha Conservative kimejiongezea hadi sasa jumla ya viti 20 na kusajili ushindi katika majimbo 279.
Chama kikuu cha upinzani Chama cha Leba kimesajili jumla ya viti 217 hii ikiwa na viti 25 chini ya idadi iliyokuwa nayo katika bunge lililopita
Huku matokeo ya theluthi moja ya maaneo bunge yakiwa yametangazwa waziri mkuu David Cameron anaonekana kurejea afisini lakini bila idadi kubwa ya wabunge ikimaanisha kuwa Chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Cameron amesema kuwa anapania kuendelea kuiongoza uingereza ya pamoja .
Shirika La BBC linakisia kuwa Cameron na Chama chake huenda wakasajili ushindi wa maeneo bunge 329.
Waziri huyo mkuu hata hivyo anawaomba wafuasi wake wasubiri hadi matokeo kamili yatangazwe.
Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland kutoka kwa chama cha kitaifa cha Scotland National Party SNP .
Licha ya Matokeo hayo Mazuri huko Scotland ambapo SNP ilisajili ushindi mkubwa wa majimbo 50 chama hicho hakikutamba katika maeneo ya England na Wales.
Chama cha The Liberal Democrats wanaelekea kusajili matokeo duni wakiwa tayari wameshinda viti vinane pekee.
Nyota wa chama hicho (Lib Dems) Vince Cable, Ed Davey na Danny Alexander wote wameshindwa katika uchaguzi huo.
BBC ilikuwa imebashiri kuwa Conservative watasajili ushindi katika maeneo bunge 329, Labour 233, the Lib Dems 8, SNP 56, Plaid Cymru 3, UKIP2, Greens 1 na vyama vyengine vidogo viti 19.

Wakenya wafwatilia uchaguzi Uingereza

Uchaguzi wa bunge la 56 la Uingereza umekuwa ukifuatilia kwa makini nchini Kenya ambapo hafla maalum imeandaliwa katika makaazi ya ubalozi wa Uingereza katika mji mkuu Nairobi.
Raia wa Uingereza wanaoishi Kenya, walijumuika na Wakenya na wanadiplomasia katika hafla hiyo mapema leo.
Walikusanyika kusubiri matokeo ya uchaguzi huku wakifuatilia matokeo kupitia televisheni zilizotundikwa kwenye bustani .
Umuhimu ilikuwa sio tu kutaka kujua mshindi katika uchaguzi huu bali pia, maslahi tofauti kwa jamii nchini Kenya kutokana na misimamo na sera tofauti za vyama vilivyogombea katika uchaguzi huu.
Hii ni pamoja na sera za nchi za nje, masuala ya kiuchumi na biashara, masuala ya uhamiaji na msimamo wa Uingereza kuhusu kusalia au kujitenga na Umoja wa Ulaya, yote haya yakiwa ni miongoni mwa ahadi walizotoa wagombea kwa wapiga kura wakati wa kampeni zao.
Miongoni mwa waliokuwepo ni aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga, ambaye ameeleza kuridhishwa kwake na namna Uingereza imefanikiwa kuanda uchaguzi huu.
Wakenya wafwatilia uchaguzi Uingereza
Amesema ni mfano mzuri kwa nchi za Kiafrika kuiga.
''Huo ni mfano mzuri ambao mataifa ya Kiafrika hayana budi kuiga kwani tofauti na Uingereza, ghasia zimekuwa zikishuhudiwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika ''
''Viongozi wengi wa Afrika hawakubali matokeo ya uchaguzi '' Alisema Bw Odinga.
Na sio tu wanasiasa, mabalozi,na wasomi walioona umuhimu wa kufuatilia matokeo ya uchaguzi huu wA Uingereza, bali pia kulikuwemo msanii wa mtindo wa Hip Hop kutoka Kenya Octopizzo.
'
Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga akizungumza na BBC 


'Nimefurahishwa sana jinsi uchaguzi huu ulivyopangwa na haswa nidhamu ya vyombo vya habari vya Uingereza''.
''Hawakutangaza chochote kuhusu wagombea na kampeni punde tu baada ya kumalizika kwa muda maalum wa kampeni na kuanza kwa uchaguzi huo''.Alisema Henry Ohanga al-maarufu OctoPizzo.
''Hilo linasaidia kuondosha ushawishi wa vyombo vya habari kwa wapiga kura'' aliongozea Octopizzo.
Wengi wanafuatilia uchaguzi huo kutokana na uhusiano wa Kenya na Uingereza .
Uingereza ni mojawapo ya nchi zenye ushawishi mwingi duniani na hivyo, sera zitakazoidhinishwa zitakuwa na ushawishi katika sehemu nyingine duniani, likiwemo bara la Afrika kwa kutegemea nani au chama kipi kitakachoingia madarakani.
Amesema ni mfano mzuri kwa nchi za Kiafrika kuiga.
''Huo ni mfano mzuri ambao mataifa ya Kiafrika hayana budi kuiga kwani tofauti na Uingereza, ghasia zimekuwa zikishuhudiwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika ''
''Viongozi wengi wa Afrika hawakubali matokeo ya uchaguzi '' Alisema Bw Odinga.
Na sio tu wanasiasa, mabalozi,na wasomi walioona umuhimu wa kufuatilia matokeo ya uchaguzi huu wA Uingereza, bali pia kulikuwemo msanii wa mtindo wa Hip Hop kutoka Kenya Octopizzo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu