INSPEKTA WA POLISI ATOA USHAHIDI KESI YA ALBINO MWANZA
Na Daniel Mbega, Mwanza
SHAHIDI
wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi
(albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa
ushahidi wake leo hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Mbele
ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka
2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na
mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.
Hata
hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14,
2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti
kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku
hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.
Washtakiwa
katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal
Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.
Marehemu
Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani
kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na
kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno
mawili ya mbele.
Brother Danny Blog (Kisima cha Hekima na Busara)
Cell: +255 - 715 - 070 109
Whatsapp: +255 - 656 - 331 974
0 comments:
Post a Comment