Friday, May 8, 2015

KITUO CHA REDIO CHA EFM CHAMKUMBUKA MWANAMUZIKI JUMA NATURE KWA MCHANGO WAKE KATIKA MUZIKI NCHINI
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha lijulikalo kama Komaa Concert  litalofanyika mwishoni mwa mwezi mei  kwa ajili ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki ya msanii Juma Nature 'maarufu Kiroboto' namna ya kuonesha kuthamini mchango wake katika muziki wa bongo fleva na kuwakumbusha watanzania juu ya safari ya muziki wa Tanzania kwa ujumla. Kulia ni mwanamuziki huyo, Juma Nature na Ofisa Habari wa kituo hicho cha redio, Lydia Moyo.

Na Dotto Mwaibale

KATIKA kusherehekea miaka 16 ya muziki kwa msanii Juma Nature, Kituo cha Radio cha EFM, wanatarajia kuungana nae kwenye sherehe hizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mahusiano Denis Sebo alisema wao ni wadau wa muziki na pia wanatambua mchango wa wasani wakongwe nchini ikiwa ni pamoja na Juma Nature.

"Leo tuna furaha kutangaza kwamba wakati Juma Nature anatimiza miaka kumi na sita kwenye game ya muziki, sherehe zake zimeunganishwa na zakwetu ili kwapamoja tufanye concert kubwa kusherekea miaka 16 ya Juma Nature," alisema Sebo.

Alisema tamasha hilo lijulikanalo kama 'Komaa Concept' ambalo litafanyika mwishoni mwa Mei,  mwaka huu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki ya msanii Juma Nature, maarufu kama 'kiroboto'.

"Hii inatuonesha tunathamini mchango wake katika muziki wa bongo fleva na kuwakumbusha watanzania juu ya safari ya muziki wa Tanzania kwa ujumla, sisi kama kituo ni wadau wakubwa wa muziki na wasani, hivyo basi tumeona ni vema kuhitimisha sherehe hizi na tamasha la komaa concert kwa sababu kwetu muziki ni nyenzo kubwa ya burudani na Juma Nature ni mmoja wa waasisi wa muziki nchini kwetu," alisema Sebo.

Alisema mchakato kuelekea tamasha hilo  utakuwa wa wiki tatu  ambapo wataangalia kwa undani zaidi muziki wa Juma Nature kwa kuangalia mistari yake ya nyimbo, maneno aliyokuwa anayotumia ,na jinsi muziki wake ulivojenga jamii , pia kumfahamu msanii huyo kiundani zaidi na kuhitimisha tamasha hilo kwa kupambwa na burudani kutoka kwa msanii huyo na burudani zingine kibao.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com/)


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu