Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akiwa na
baadhi ya watendaji wa Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa
nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia
kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na
shirika hilo katika vituo vya Afya 13.
*
Dk Seif Rashid, Waziri, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, mgeni rasmi katika
hafla ya uzinduzi *
(6 Mei 2015, Dar es Salaam, Tanzania na New York, Marekani) - Katika
hafla ya leo jijini Dar es Salaam, World Lung Foundation (WLF) Tanzania
ilizindua mradi wa elimu kwa njia ya mtandao katika hatua mpya ya kusaidia
kuboresha ubora wa huduma za wajawazito pamoja na akina mama na watoto wao.
Mradi huu wa Mawasiliano umefadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Sweden (Swedish
International Development Cooperation, (Sida)) na Shirika la Merck For Mothers.
Mradi huu upo katika vituo vya afya 13 vinavyo fadhiliwa na WLF katika mikoa ya
Kigoma, Pwani na Morogoro.
Mfumo huu wa WLF Tanzania
wa elimu kupitia mtandao (e-learning)
umeundwa ili kuboresha ujuzi wa wafanyakazi
wa vituo vya afya na kuongeza wao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika
kliniki zitoazo huduma za afya. Mfumo huuutawasaidia kufanya maamuzi ya kitaalam kuhusu usimamizi
wa dalili hatarishi za ujauzito, huduma wakati wa kujifungua na baada ya
kujifungua kwa ajili ya akina mama na watoto wao.Mafunzo haya yatawawezesha
watoa huduma ya afya kuwasiliana na kupata taarifa muhimu za kuongeza ujuzi, kusoma
Makala za jarida za kitaalam, kuona filamu zinazoelimisha, picha na masomo ya
kujifunzia. Wafanyakazi wa afya pia
wanaweza kutumia jumuishi ya vikao vya mitandao na kubadilishana ujuzi na
taarifa kuhusu changamoto na mafanikio
yao pamoja na wenzao na wataalam
waandamizi katika vituo vya afya 13.
“Tunaiomba serikali kuharakisha upatikanaji
wa mtandao yaani intaneti vijijini ili tuweze kuunganisha vituo vya afya kupitia
mkongo wa taifa, ili vituo vingi vya afya viweze kutumia mradi huu kwa njia ya
gharama nafuu, "alisema Dk Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi wa Tanzania, World Lung Foundation.
"Uwekezaji kama huu unaweza kusaidia kuokoa maisha ya mama wengi zaidi na
watoto wao."
Programu hii ya elimu kwa njia ya mtandao ni maendelezo ya
uboreshaji unaofanywa na WLF na sehemu ya mkakati wa matumizi ya miradi wa ICT
ili kusaidia kuboresha matokeo ya afya.
Jamii
ya huduma na kujifunza
Vituo 13 vya afya vilivyounganishwa na
mfumo huu ni pamoja na Kituo cha Afya cha Kibiti na Hospitali ya Wilaya Utete
katika wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani. Katika Mkoa wa Morogoro, vituo vya afya
ni pamoja na Kituo cha Afya cha Mlimba kilichopo katika wilaya ya Kilombero ,
na Mtimbira na Mwaya vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya ya Mahenge Ulanga.
Katika mkoa wa Kigoma, vituo vya afya ni pamoja na Kituo cha Afya Nguruka
katika wilaya ya Uvinza, Kituo cha Afya cha ujiji na Hospitali ya Mkoa Maweni
Kigoma mijini wilaya, Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, Hospitali ya Wilaya ya
Kibondo na Mabamba Kituo cha Afya katika Kibondo wilaya na Kakonko Kituo cha
Afya katika wilaya ya Kakonko . Pamoja na haya, vituo viwili vyaafya katika
mkoa wa Kigoma - Kituo cha Afya cha Buhingu katika wilaya ya Uvinza ya na Kituo
cha Afya cha Nyenge katika wilaya ya
Kasulu – wataunganishwa na mpango huu mbunifu wakati marekebisho ya kiufundi yatakapokamilika.
|
0 comments:
Post a Comment