Saturday, June 6, 2015

CHADEMA YATISHA ARUSHA

 Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"
 Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura"
Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha  AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
 umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha
Mjumbe wa Kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum Mh Grace Kiwelu amewataka Wanawake kuwa Chachu ya mabadiliko kwa Taifa letu."MUDA WA KUDANGANYWA KWA KANGA UMEPITA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI OCTOBER TUPATE UHURU WA UHAKIKA,WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZA"

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na Chadema Kanda Ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za Hamasa ya kujiandikisha kanda ya kaskazini amewaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndio imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili October tufanye maamuzi sahihi

Mbunge wa Rombo Joseph Selasini" WATANZANIA WENZANGU HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OCTOBER TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIO SAFARI YA MATUMAINI"

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mh Pauline Gekul awatakwa Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi wetu kwa kutumia simu mitandao ya kijamii vikao vya kijamii ili ifikapo October tuiondoe CCM madarakani.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI

 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Rebecca Mgodo amewataka wananchi kusoma nyakati"NDUGU ZANGU MIAKA YA MATESO KWA WATANZANIA SASAS IMEFIKA MWISHO, TWENDENI KWA UMOJA WETU TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURATUITOE CCM MADARAKANI"-Mgodo

Mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Kaskazini Mh Israel Natse akiwaongoza viongozi na Wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuingia uwanjani huku wakiwapungia wanachama na wapenzi wa Chadema waliofika uwanjani vya kilombero (PICHA NA WOINDE SHIZZA) LIBENEKE LA KASKAZINI
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu