Thursday, June 4, 2015

KURESHI UFUNGUO KUANZISHA SOKA YA WATOTO

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kureshy Ufunguo (Kushoto) akioneshwa mipira inayofaa kwa ajili ya kufundishia watoto kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally (Picha na Mpiga Picha Wetu.)


Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Kureshy Ufunguo (Kulia) akipokea jezi kwa ajili ya kuanzisha shule ya mafunzo ya watoto wadogo (Picha na Mpiga Picha Wetu).

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally (Kulia) akimkabidhi vifaa vya kuweka alama uwanjani wakati wa mafunzo mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Kureshy Ufunguo aliyeamua kuanzisha shule ya watoto.

Na Mwandishi Wetu
MCHEZAJI wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simba, Kajumulo na Mirambo ya Tabora, Kureshy Ufunguo ameamua kurudi uwanjani safari hii kuanzia Soka ya Watoto (Academy) ili kusaka vipaji vya wachezaji wa kuunda Stars baadaye.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kureshy ambaye aliwahi kuchezea Stars kwa nyakati tofauti alisema anaona uchungu kuona timu ya Taifa inafanya vibaya mara kwa mara wakati kuna watoto wengi wenye vipaji ambavyo vikiliendelezwa vitaibua wachezaji wazuri.
Alisema amefanya mazungumzo na baadhiu ya maduka ya kuuza vifaa vya michezo likiwemo Isere Sports na kuchagua vifaa ambavyo ataanzia katika kufundisha watoto hao.

Kureshy alisema kwa kuanzia atakuwa anawakusanya watoto katika Klabu aliyoianzisha Kitunda, Kivule ambapo ataanza kuwafundisha kwa nadharia yaani darasani na baadaye uwanjani ambako atatumia uwanja wa Shule ya Sekondari, Misitu, Kivule Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally alisema Kampuni yake itasaidia kutoa vifaa vya kuanzia mazoezi kama vikinga ugoko (shin guard), mipira na jezi za mazoezi.
Alisema Kampuni itaendelea kutoa misaada kwa mchezaji huyo kwani ni wachache wenye ndoto ya kufufua soka ya Tanzania ambayo kwa sasa Stars haifanyi vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Kureshy Ufunguo (Kulia) akiangalia kikombe kwa ajili ya zawadi wa timu katika mashindano mbalimbali (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu