2


SI LA KULIKOSA

Wednesday, June 3, 2015

IKIWA ni siku moja tu baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa tano kuliongoza Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, FIFA, Rais wa Shirikisho hilo, Sepp Blatter (79), (pichani), amejiuzulu wadhifa huo, leo Jumanne Juni 2, 2015
Tayari ametangaza kuitishwa kwa mkutano mkuu  haraka iwezekanavyo, ili apatikane mrithi wake.
Kujiuzulu kwa Blatter, ni sawa Mbuyu kuanguka, yalianza matawi na sasa Mbuyu wenyewe, kwani wiki iliyopita, viogogo kadhaa wa shirikisho hilo, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kupokea mlungula.
Akitanagza uamuzi huo baada ya kuita mkutano na waandishi wa habari, Blatter alisema, “Maslahi ya Fifa, ndiyo mapenzi yangu, na ndiyo sababu nimeamua kuchukua uamuzi huu, kinachohesabika hapa kwangu mimi ni taasisi ya FIFA na mpira wa miguu duniani kote.” Alisema Blatter wakati akitrangaza uamuzi huo mjini Zurich, UswisShare this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu