MWANDISHI wa habari mkongwe, ambaye
amejishindia tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya CNN, Richard Mgamba,
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Limited,
na tayari amekwisha kabidhiwa "mikoba" na aliyekuwa akikaimu nafasi
hiyo, Bi.oyce Mhavile, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One.
Mhavile alikuwa kikaimu nafasi hiyo, baada ya
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake,
Kiondo Mshana, kustaafu kwa mujibu wa sheria. Mara ya mwisho Mgamba
akikjuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Citizen. Pichani Mgamba,
akionyesha alama ya dole, ikiwa ni ishara ya ushindi, baada ya kunyakua
tuzo ya CNN mwaka 2008
0 comments:
Post a Comment