Tuesday, August 4, 2015


CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimemteua rasmi Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Edward Ngoyai Lowassa, kuwa mgombea wake rasmi wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho ulioketi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Agosti 4, 2015, ulimteua Mh. Lowassa kuwa ndiye atakuwa mgombea wake wa Urais na kwa hali hiyo anakuwa mgombea rasmi wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, unaoundawa na vyama vya upinzani vya CUF, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na NLD.
Hali kadhalika, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF, Zanzibar, Juma Duni Haji, amekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA na baadaye kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Mh. Lowassa. Hii ni kufuatia makubaliano ya UKAWA, ambapo mgombea mwenza ni sharti atoke CUF, ingawa matwaka ya kikatiba yanaelekeza kuwa mgombea Mgombea mwenza wa kiti cha Rais, ni lazima atoke chama kimoja na mgombea mwenza na hivyo Mh. Duni Haji akalazimika kukihama chama chake. Mh. Lowassa amabye alikihama chama chake cha zamani CCM na kujiunga na UKAWA, hatua hiyo imebadilisha sura ya siasa za Tanzania, kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, ambapo wanasema, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na ushindani mkubwa, kwa vile vyama vikuu vya uopinzani vimeamua kuungana na kjusimamisha mgombea mmoja kwa kila eneo, la Ubunge, Udiwani, Uwakilishi na Usheha.
Mh. Lowassa na Mh. Juma Duni Haji, walichaguliwa kwa kura ya wazi, ambapo wajumbe wa mkutano huo kupitia kanda zao waliulizwa kama wanawachagua au la  na wote waliitikia kukubali kuwachagua.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, (wasita kushoto), Mgombea urais wa chama hicho, Mh.Edward Lowassa, (watatu kulia), Mgombea mwenza wa Mh. Lowassa, Juma Duni Haji, (wanne kushoto) na wanachama wapya wa chama hicho waliojiunga wakitokea CCM wakishikana mikono kuonyesha mshikamano

Mtoto mkubwa wa Mh. Lowassa, Freddy (katikati), akiwa na marafiki zake, wakifuatilia mkutano huo
               Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
Vijana wa 4U wakishangilia na kuonyesha mabango yanayomsifia Mh. Lowassa
                   Wageni waalikwa kutoka mataifa ya nje
      Mh. Lowassa, (kushoto), mgombea mwenza Juma Duni Haji na     mgombea kiti cha Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu