SHULE YA MSINGI KIBULUGWA MBAGALA YANUFAIKA NA MADAWATI 100 TOKA KCB TANZANIA
Meneja
Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City Jijini Dar es
Salaam, Benjamin Mgonja akiangalia daftari la Mwanafunzi wa darasa la
sita katika shule ya msingi Kibulugwa ya Mbagala jijini Dar es Salaam
John Mwaipopo(watano toka kushoto)wakati wa hafla fupi ya makabidhino
ya msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na
kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini
Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa darasa la sita wa shule ya msingi Kibulugwa ya Mbagala jijini Dar es
Salaam,kutoka kushoto Mwajuma Abdallah,Khalima Khalfan na Mwanaid
Mwakipesile wakimsikiliza kwa makini Ofisa Uhusiano na wateja wa benki
ya KCB Tanzania,Victoria Kisima akiwafafanua jambo liloandikwa katika
daftari wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya msaada wa madawati 100
kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa
madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule msingi Kibulugwa ya Mbagala jijini Dar es Salaam
wakiwa wamekaa kwenye madawati 100 waliyopewa msaada na benki ya KCB
Tanzania wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya msaada wa madawati
hayo kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa
msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Kibulugwa ya Mbagala jijini Dar es
Salaam wakibeba madawati kuyapeleka madarasani baada ya kukabidhiwa
rasmi msaada wa madawati 100 na benki ya KCB Tanzania ikiwa ni sehemu
ya mradi wa madawati 1000 kwa shule za msingi 10 za msingi jijini Dar es
Salaam
0 comments:
Post a Comment