Thursday, February 11, 2016

AJALI YA BASI LA SIMBA MTOTO LAPOTEZA MAISHA YA ABIRIA 11 TANGA NA KUJERUHI 29.



Tanga. Watu 11 wamefariki dunia leo huku wengine 29 wamejeruhiwa baada ya Basi la Simba Mtoto kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Pangamlima wiliyani Muheza. 

Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa Basi la Simba Mtoto lilikuwa linatokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam. 
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2016/02/SI2.jpg 
Kamanda Mihayo ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea mapema leo baada ya dereva wa lori kuhama njia na kukutana uso kwa uso na basi hilo. 

Pia kamanda Mihayo amesema kuwa, kati ya watu 11 waliopoteza maisha ni pomoja na madereva wa magari hayo mawili. 
Kamanda Mihayo ameongeza kuwa majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Muheza huku jitihada zikifanyika kuwapeleka abiria watano ambao hali zao ni mbaya katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi mkoani Kilimanjaro
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu