2


SI LA KULIKOSA

Thursday, February 18, 2016


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.


Fundi wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda hicho.Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu