2


SI LA KULIKOSA

Thursday, February 25, 2016Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba yake, Joyce alimpongeza Rais John Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka katika Serikali yake. Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrsion Mseke
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza

Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke akizungumza katika hafla hiyo


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya kumaliza sherehe fupi iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo
picha ya pamoja
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu