2


SI LA KULIKOSA

Wednesday, March 9, 2016AJALI MBAYA YATOKEA LEO ALFAJIRI TABATA - MATUMBI JIJINI DAR ES SALAAM

Muonekano wa basi la abiria aina ya DCM baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika barabara ya Tabata - Matumbi jijini Dar es Salaam mapema leo alfajiri. 

Watu wawili mpaka sasa wamefariki dunia huku watu wengine wengi wakijeruhiwa baada ya magari matatu kugongana leo saa kumi na moja na nusu alfajiri katika eneo la Tabata - Matumbi. 

Taarifa za awali zinasema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni lori la mchanga kuligonga basi la abiria aina ya Dcm kwa nyuma, kisha basi hilo kuruka upande wa pili wa barabara baada ya dereva wake kupoteza uelekeo na kugongwa tena na lori lingine aina ya Scania na kusababisha vifo na majeruhi. 
                                                                              Askari polisi wakiwa eneo la ajali
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu