Thursday, March 17, 2016

HOSPITALI YA KAIRUKI KUTIMIZA MIAKA 29 YA KUTOA HUDUMA ZA AFYA

indexMkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki,Dk.Asser Mchomvu .KAI1 KAI2 KAI3 Na Mwandishi wetu
................................
Hospitali ya Kairuki (KH) inatimiza miaka 29 mwezi huu siku ya Alhamisi tangu ilipoanzishwa tarehe 17.03.1987.
Akizungumzia maadhimisho hayo Dr Asser Mchomvu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki anasema kuwa uongozi wa KH unapenda kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nao katika kuiwezesha KH kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wote.
Dr Mchomvu anaongeza kuwa katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali kwa kufikisha miaka 29, KH itafanya maadhimisho yake kwa kutoa msaada kwa vituo vya afya pia kufanya upimaji wa kinywa na meno bure. “Madhimisho haya yataambatana na utoaji wa vifaa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, ambapo KH itatoa msaada wa vitanda vya hospitali na magodoro siku ya Alhamis tarehe 17.03.2016,” alisema Dr Mchomvu Alisisitiza kuwa pamoja na hilo, KH itatoa pia huduma ya upimaji na ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa wananchi kwa siku mbili bure ( siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 16 na 17, Machi 2016) kuanzia saa 2 asubuhi, pale pale Hospitali ya KAIRUKI, Mikocheni, Dar es Salaam.
Dr Mchomvu anaeleza kuwa, kutakuwa na ghafla fupi ambapo Mkurugenzi atatoa salamu baada ya kukata keki na watoto waliozaliwa KH mwaka 1987. Watu wote wanakaribishwa katika ghafla hiyo itakayofanyika hapo KH siku hiyo ya Alhamisi tarehe 17.03.2016 saa 10 jioni.
Kwa upande mwingine KH imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zake huku ikizingatia ufanisi na ubora katika utowaji wa huduma zake kwani inatumia vifaa vya kisasa ambavyo vina ubora wa hali ya juu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu