2


SI LA KULIKOSA

Monday, March 7, 2016

kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimlisha keki mkurugenzi mwenzake, ambae ni (mme wake) ndugu Kim Godwin Fute,alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.

Mhandisi Balozi John William Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi mpya
NA K-VIS MEDIA
ILE "fagia fagia" ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo hii Machi 6, 2016 imehamia Ikulu, tena ofisini kwake kwa msaidizi wake wa karibu, Balozi Ombeni Sefue, ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Taarifa fupi ya Ikulu yenye mistari mitano iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa haikueleza sababu hasa za mabadiliko hayo ya ghafla ikiwa ni chini ya miezi mitatu tangu balozi Sefue ateuliwe kuendelea na nafasi hiyo nyeti.
Rais katika taarifa hiyo ya Ikulu, amesema atampangia kazi nyingine baloziSefue, huku akimteua Balozi wa Tanzania nchini
India, Mwanadiplomasia ambaye pia ni Mhandisi, John William Kijazi kushika wadhifa huo.  
Wiki iliyopita Serikali kupitia Idara ya Habari Maelezo, ilikanusha vikali tuhuma zilizoelekezwa kwa balozi Sefue kuwa ameingilia utoaji kandarasi kwenye makampuni ya ujenzi. Katika kanusho hilo, Serikali ilionya waliosambaza taarifa hizo kukanusha mara moja tena kwa uzito ule ule vinginevyo hatua kali zingefuatia. Balozi Sefue anakuwa "Mhanga"wa kwanza wa ngazi za juu serikalini kupitiwa na "Panga" la Rais Magufuli ambaye yeye binafsi anaita ni kazi ya kutumbua "majipu".Balozi Ombeni Sefue, sasa kupangiwa kazi nyingine
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu