Monday, April 11, 2016

MKUU wa mkoa wa Shinyanga, Anna Kilango Malecela (pichani),  amekuwa muhanga wa kwanza wa ngazi ya ukuu wa mkoa, kufukuzwa kazi mapema na Rais Dkt.John Pombe Magufuli, bàda ya kuutangazia umma kuwa mkoani kwake hakuna watumishi hewa. Ikulu baada ya kusikia hivyo ikianzisha uchunguzi wake na kugundua kuwa Mkuu huyo wa mkoa "alikurupuka", kwani taarifa yake haikuwa ya kweli. Kufuatia mapungufu hayo, Leo April I 11, 2016, Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wake kama Mkuu wa mkoa. Halikadhalika Katibu Tawala wa mkoa huo nae amefukuzwa kazi kwa kosa hilohilo, na muchunguzi dhidi yao uneanzishwa.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu