Bingwa wa Kombe la Mama Shija kuzawadiwa medali 15 za dhahabu
Na Mwandishi Wetu
TIMU
ya soka ya Wamang'ati FC ya Mbagala inaingia uwanjani leo kupambana na
Uswahilini kwenye fainali ya mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la
Mama Shija zitakazofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingugi, Mbagala
Kiburugwa.
Muandaaji
wa mashindano hayo, Fatuma Shija alisema jana Dar es Salaam kuwa
maandalizi ya fainali hizo yamekamilika ikiwepo kuandaa zawadi za
washindi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Fatuma Mjema.
Alisema
bingwa wa mashindano hayo ataondoka na zawadi ya Kikombe, Medali 15 za
dhahabu, jezi seti mbili, mpira mmoja na mshindi wa pili atapata zawadi
ya jezi seti mbili, mpira mmoja na medali 15 za fedha huku mshindi wa
tatu atapata jezi seti moja na mpira mmoja.
Mama
Shija alisema lengo la mashindano hayo ni kuwaweka pamoja vijana
kutumia muda wao mwingi kujihusisha na michezo na kuibua vipaji vingi
vya vijana watakaunda timu ya soka ya wilaya mpya ya Kigamboni.
Alisema
baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yatafuata mengine baaada ya
miezo minne ikiwa ni mfululizo wa michezo kwa vijana.
Kabla
ya fainali hizo kutakuwa na fainali nyingine za mchezo wa bao kati ya
mabingwa wa mchezo huo kutoka Kilungule, Kiburugwa na wenyeji Kinguge.
mwisho
0 comments:
Post a Comment