2


SI LA KULIKOSA

Thursday, April 28, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Jumanne Abdallah Sagini (kulia) kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu akisaini Hati ya kiapo chake mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Selestine Muhochi Gesimba kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Geita leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Thea Medard Ntara kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhandisi Zena Said kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo cha Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Albert Gabriel Msovela kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendendea kazi Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Gabriel Msovela mara baada ya kumwapisha, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Angelina Mageni Lutambi kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Singida leo, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa 10 walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Wengine pamoja nae ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi, Balozi John William Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa 10 Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Makatibu Tawala wa Mikoa wakiapa mara baada ya kujaza Fomu za maadili kwa viongozi wa umma zinazowataka kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makatibu Tawala wa Mikoa wakijaza Fomu za maadili ya Viongozi wa Umma zinazowataka kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya kujaza Fomu za maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu jijini Dar es salaam.


Na. Waandishi Wetu - Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Makatibu Tawala wapya wa mikoa 10 aliowateua Aprili 25 mwaka huu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi.

Makatibu Tawala walioapishwa leo ni Bw. Jumanne Abdallah Sagini ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Selestine Muhochi Gesimba Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Geita na Dkt. Thea Medard Ntara Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tabora.

Wengine ni Mhandisi Zena Said ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Albert Gabriel Msovela Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Angelina Mageni Lutambi aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Singida, na Dkt. Angelina Mageni Lutambi ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida.

Pia amewaapisha Bw. Richard Kwitega kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Arusha, Bw. Armatius C. Msole kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Aisha Amour ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro na Bw. Zubeir Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani.

Mara baada kuapishwa Makatibu Tawala hao wamejaza fomu za Maadili kwa viongozi wa umma zinazowataka wazingatie Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma.

Akizungumza na Makatibu Tawala hao mara baada ya kukamilisha zoezi la ujazaji wa fomu hizo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amewataka wazingatie maadili na mipaka yao ya kazi na kuepuka kuwabagua watumishi wanaowaongoza.

Balozi Kijazi amewataka waishi kwa kufuata miiko na maadili kwa viongozi wa umma yaliyoanishwa kwenye fomu walizojaza ili kuepusha mgongano wa kazi na maslahi mahali pa kazi.

Amewaagiza Makatibu Tawala hao kuwasimamia watumishi walio chini yao ili maadili waliyokubali kuyazingatia yafuatwe na watumishi walio chini yao.
“Napenda kuwajulisha kuwa tuko kwenye awamu nyingine, na mnajua kuwa awamu hii ikisema jambo maana yake litekelezwe, msije mkaliacha mezani na kuendelea na mambo mengine” Amesisitiza Balozi Kijazi.

Amewataka Makatibu Tawala hao kushirikiana kikamilifu na watumishi wanaowaongoza ili waweze kutatua kero mbalimbali za wananchi kwa kuyashughulikia kwanza matatizo watakayoyakuta katika vituo vyao kabla ya kuanzisha mambo mapya.

Kwa Upande wao Makatibu Tawala walioapishwa wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamejipanga kikamilifu kutekeleza kwa vitendo Kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo waliyopangiwa.

Bw. Zubeir Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Pwani amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuwa anashirikiana na watumishi wenzake kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Pwani.

Amesema kuwa ataweka mkazo katika kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo ya kiuchumi, kukuza sekta ya kilimo cha mazao ya Chakula, Biashara na Elimu mkoani Pwani.

Aidha,amesisitiza kuwa anakwenda kulisimamia kikamilifu suala la uhakiki wa Watumishi hewa katika mkoa wake pamoja na kushughulikia migogoro ya ardhi iliyo katika mkoa wa Pwani.

Naye Dkt. Angelina Mageni Lutambi ambaye aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida akizungumza mara baada ya kuapishwa amesema kuwa jukumu lililo mbele yake ni kuhimiza uchapakazi miogoni mwa watumishi wa mkoa wa Singida.


“Nimelipokea jukumu hili nililokabidhiwa na Mhe. Rais kwa Moyo wa dhati, nitahakikisha kuwa ninawatumikia wananchi na kuwahimiza viongozi wenzangu kutimiza wajibu wao ipasavyo” Amesisit


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifungua, Mkutano wa Watunza kumbukumbu Jijini Dar es Salaam leo (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mshauri Mkuu wa Chama cha wataalamu hao na Afisa kumbukumbu na Taarifa za Afya Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Geofrey Semu akizungumza na washiriki hao kabla ya kufunguliwa Mkutano huo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo mkutano huo unatarajiwa kufungwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki kutoka Mikoa Mbalimbali Tanzania wakisikiliza kwa makini wakati wa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokua akizungumza leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wenyeji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wageni kutoka Mikoa mbalimbali Tanzania wakisikiliza kwa umakini
Baadhi ya washiriki toka Mikoa Mbalimbali wakimsiliza Mkuu wa Mkoa Paul Mamonda (hayupo pichani) na mwenyeji mwenyeji wao, Elizabeth Mlindoko (wa pili kulia) kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI)

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji ,
Maeneo mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu